Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,829
- 6,287
Kuna tofauti kubwa sana za utashi na utendaji kati ya hayati JPM na mama SSH.
JPM, alijitahidi sana kuishi maisha ya watanzania. Namaanisha watanzania walio wengi. Wenye hali inayoendana na uchumi wa nchi inayoitwa 'maskini'
Ndio. Huwezi kufananisha uchumi wa nchi tajiri au kudhani kwamba wananchi wako wanaishi maisha sawa na nchi tajiri kwasababu tu wewe ni raisi wa nchi.
Kuwa rais au kiongozi mkuu wa nchi hakuondoi hali duni za wananchi walio wengi.
Kuna watanzania hawana barabara, maji, umeme, huduma za afya, na hata mfumo wa elimu ni duni; wanabanana darasani au hata kukaa chini.
Hawa hawawezi kuwa sawa na nchi zilizoendelea. Kipato chao hakiwezi hata kidogo kufananishwa na kile cha wananchi wa nchi zilizoendelea.
Kudhani kwamba maisha ya watanzania wachache wanaotembelea v8 au magari mengine ya kifahari, wanaofanya sherehe za kuzaliwa kwa gharama kubwa, wanaosomesha watoto wao shule za gharama kubwa, kwamba ndio maisha ya watanzania wote, huko ni kudanganyana.
Hata hivyo, kuzungumza lugha kama wanayozungumza wao, haitufanyi kuwa sawa nao. Na ndio maana tunaitwa 'nchi maskini' zinazotegemea msaada kutoka kwao. Hatuwezi kuwa sawa nao kwasababu tu, tunakaa na kula pamoja nao!