Hayati Ali Hassan Mwinyi alikuwa hadithi nzuri na ya mfano miongoni mwa Watanzania

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
1,049
3,084
Nilikuwa darasa la pili mwaka 1992, Shule ya msingi Bungo pale Morogoro mjini, nilipomuona kwa mara ya kwanza Rais Ali Hassan Mwinyi akishuka kwenye helkopta viwanja vya Gymkhana kuelekea uwanja wa Jamhuri kwenye sherehe ya Mei Mosi, niliendelea kumsikia kwenye taarifa ya habari na kumsoma kwenye magazeti.

Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa hadithi nzuri miongoni mwa jamii kutokana na unyenyekevu wake mbele za Mwenyezi Mungu, alikuwa Kiongozi kipenzi cha watu wengi sababu ya ucheshi wake, upole wake, unyevunyevu wake,mtu asiyependa makuu, mtu hasiyependa dhuluma na mpenda maendeleo.

Tunamuombea dua ili Mwenyezi Mungu amuondolee adhabu ya kaburi na akufufue tena siku ya mwisho.

Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa Kiongozi kweli kweli wa namna ya pekee, hakuwa mdini wala mkabila, aliwachukia wadini wa wakabila, mfano wahuni walipoanza kuvunja mabucha ya nguruwe kwa kisingizio cha dini, Rais Mwinyi akatangaza rukhsa mtu yoyote kula kitu chochote, hakuna ruhusa ya mtu mwingine yeyote kuingilia uhuru wa mtu wa dini nyingine yoyote kula chochote, “Ruksa” na huo ukawa ndio mwanzo wa kuitwa Mzee wa Ruksa.

Wale wahuni kwa kisingizio cha dini walishughulikiwa kikamilifu, Ruksa nyingine kubwa Rais Mwinyi aliyotuachia ni ruksa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania kiasi kwamba sifa ya Baba wa demokrasia Tanzania inamstahili kabisa! Mwinyi ndie Deng Xioping wetu.

Deng alikuwa Kiongozi mkuu wa Taifa la China, alifanya Mabadiliko mengi kiuchumi ikiwamo kuanzisha vyuo vya ufundi nchini China, nae ni Mzee rukhsa wa China kama ilivyo hapa kwetu kwa Hayati Rais Ali Hassan Mwiny.

Baada ya kuzifungulia hizo ruksa, alikuja kufungulia ruksa nyingine nyingi za biashara, Uchumi, akaruhusu mitumba, akaruhusu Chai Maharage ziwewe kuhudumia Wananchi, tukumbuke enzi hizo palikuwa na taksi tu mjini na kama unavyojua bei ya taksi ilikuwa kubwa kuliko bei ya chai maharage.

Hayati Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya CCM, Ali Hassan Mwinyi alikuwa muungwana sana,kama alivyokuwa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ndivyo alivyokuwa Hayati Ali Hassan Mwinyi,aliita nyeupe ni nyeupe na nyekundu ni nyekundu, alimpa mtu sifa yake na alikuchagua kwa sababu ya uchapakazi wako.

Hayati Ali Hassan Mwinyi, alimpenda sana Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa sababu ya uchapakazi wake, na alidiriki kusema Rais Magufuli amefanya mengi na makubwa kutuzidi sisi wote Marais watatu tuliomtangulia, mambo aliyoyafanya Magufuli ni mengi na macho yetu yanaona na masikio yanasikia, kwani ni uongo?

Hayati Ali Hassan Mwinyi aliwahi pia kuzungumzia uteuzi wa Joseph Sinde Warioba kuwa Waziri Mkuu mwaka 1985 baada ya uchaguzi mkuu akiwa kijana wa miaka 45 na kwamba kuna madai ya kushinikizwa na Mwalimu Nyerere kumteua Warioba lakini anasema uamuzi huo aliufanya yeye mwenyewe kwani alimfahamu Warioba kwa uwezo wake.

Pumzika kwa Amani Hayati Ali Hassan Mwinyi,tulijifunza unyenyekevu na kuishi bila kujiinua "low plofile" toka kwako, tunakuombea Dua Ili Mwenyezi Mungu akuondolee adhabu ya kaburi na akufufue tena siku ya mwisho.

Nikiishia hapa, mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Mwaka 1987 (akiwa na miaka 62) alikuwa na kashfa ya kutembea na msichana wa sekondari (Jangwani) . Azania wakawa wanamuita shemeji.

Lisemwe na hili.
 
Mwinyi ndie Deng Xioping wetu!. Deng alikuwa Kiongozi mkuu wa Taifa la China,alifanya Mabadiliko mengi kiuchumi ikiwamo kuanzisha vyuo vya ufundi nchini China,nae ni Mzee rukhsa wa China kama ilivyo hapa kwetu kwa Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi,
Hakuna ulinganisho wowote, hawafanani kwa lolote.
 
Nilikuwa darasa la pili mwaka 1992, Shule ya msingi Bungo pale Morogoro mjini, nilipomuona kwa mara ya kwanza Rais Ali

-Bachelor of business administration in International business

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
Okay sawa ndugu yetu, lakin tunatumain, mzee Mwinyi aliomba msamahaa kwa Mungu ili hadith yake iwe nzuri:Tunatambua mzee Mwinyi aliomba msamahaa wa kuuza Loliondo: Na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari,Katabaro aliyetoa taarifa hiyo.

Tunatambua mzee Mwinyi aliomba msamaha kwa kutorosha Nyara za, serikali kwa kushirikiana na mkewe mama Siti. Nyaraka hizo zilikamatwa na marehemu Mrema Lyatonga. Tunatambua mzee, Mwinyi aliomba msamahaa kwa kumruhusu Mohammed Enterprise, ambaye ni baba wa MO kuingiza nchini mchele mbovu.

Na mkemia, Venus Fupi aliposema ni mchele ni mbovu aliuliwa. Tunaamini aliomba msamahaa, ili hadithi iwe nzuri.Pamoja na kumsifia,sana lakin tunatambua kuwa mzee Mwinyi aliomba msamahaa kwa kuruhusu nchi iongozwe na mkewe mama Siti. Tunaamini kuwa,aliomba msamahaa.Tunamwombea kwa Mungu, na tumechukua mazuri yake.
 
Back
Top Bottom