Haya yanayotumbuliwa ni majipu au ni chunusi ?

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Japo sikubahatika kusoma lakini ELIMU YANGU ya kujua kusoma na kuandika imeniongoza kuuliza hili swali.

Rais wakati anazindua Bunge aliahidi kuwa atashughulika na wahujumu uchumi kwa kujipachika cheo cha mtumbua majipu. Ukweli nilifurahishwa na kauli hiyo japo sijaona wala kusikia jipu hata moja alilotumbua, naona vichunusi na viupele ndio anaviminya. Au anafuata Bloom Taxonomy inayosema Simple to Complex ?Kama makontena yaliporwa he waziri aliekuwa anahusika na uchukuzi yupo hai ? yeye si jipu ? waziri WA fedha wa enzi hizo yupo ? Hana kesi ya kujibu ?Kama hawa wanastaafu salama kwanini hata hao walio chini yao waliosimamishwa kazi wasiache kusumbuliwa ?

Natania tu jamani nisije cyber crime ikanizoa. Utani tu
 
Wote wameshahojiwa Na wamejitetea ya Kuwa walikuwa wakitumiwa vimemo Ili deal lifanyike,Sasa hao watoa hivyo vimemo hawagusiki.
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…