Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,376
- 78,024
Kitendo cha Jeshi la Polisi kuruhusu maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo, Jumatano Januari 24.2024 ni ishara ya utekelezaji wa falsafa ya 'R4' iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo inatajwa kuimarisha Demokrasia na umoja Nchini
CHADEMA imepanga kufanya maandamano hayo jijini Dar es Salaam ikidai marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Katiba Mpya
Kabla ya Rais Samia kuingia madarakani mwezi Machi 2021, maandamano ya upinzani na mikutano ya hadhara ilipigwa marufuku na Polisi Nchini lakini katika hali ambayo haikutarajiwa Polisi wametoa ruhusa kwa CHADEMA kufanya maandamano yao ya leo kwa amani na kuwaahidi ushirikiano
Hata hivyo, Polisi wamewapa Viongozi wa CHADEMA masharti manne ili kuhakikisha kuwa maandamano hayo yanafanyika salama
Masharti hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa waandamanaji hawaleti uvunjifu wa amani au kusababisha mali za watu kuibiwa na kuharibiwa, Viongozi na mashabiki wa Chama hicho cha upinzani pia wameonywa na Polisi kuwa wasitumie lugha za uchochezi na kejeli ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani au makosa ya jinai
Pia waandamanaji wameambiwa wafuate njia zilizokubaliwa na muda uliopangwa ili kuepusha kusababisha foleni na tafrani Barabarani
Kufuatia hatua hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake wa maridhiano wa kuruhusu maandamano hayo
"Big up kwa Polisi, tunawaahidi amani mwanzo mwisho, Big up sana pia kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hili" -Sugu
Sugu ameongeza kuwa Rais Samia ameonesha kuwa hana hulka ya kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuminya demokrasia Nchini
Naye, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amewapongeza Polisi chini ya Rais Samia kwa ushirikiano wao kwa chama chake
"Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa busara hii, karibuni Watanzania wote, tuandamane kwa amani" -Mbowe
Falsafa ya R4 (Reconciliation, Resilience, Reforms na Rebuilding of the Nation) ya Rais Samia imebadili upepo wa siasa nchini
Hii siyo mara ya kwanza kwa Serikali ya Rais Samia kuruhusu maandamano ya upinzani kwani mwezi Mei mwaka jana, Polisi jijini Dar es Salaam waliruhusu maandamano ya Umoja wa Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kwenda Ofisi za Bunge na kuwapatia ulinzi
Rais Samia ameimarisha Demokrasia kwa kuruhusu maandamano, kuruhusu vyama vya upinzani vifanye mikutano ya hadhara nchi nzima na ameimarisha usalama na kufanya wanasiasa wa upinzani waliokimbia nchi kurejea nchini
Rais Samia pia ameongeza uhuru wa wananchi wa kuongea, uhuru wa vyombo vya habari na asasi za kiraia
Aidha, Wananchi kadhaa wakitoa maoni yao kupitia kwenye mitandao ya kijamii wamemtaja Rais Samia kama 'Mama wa Demokrasia' wa Tanzania kwa uongozi wake wa maridhiano
Chadema wananufaika sana na falsafa hii ya 4R. Maana kwa sasa wanaandamana na kupewa ulizi. Hii inaitwa ukomavu wa kisiasa wa Rais wa Tanzania.
Haya ndiyo matokeo ya 4R.
4R ni nini?