Haya ndiyo maajabu ya team kiba kwa diamond

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,472
25,397
Habari zenu wanajamvi ?
Kwa upande wangu mm ni mzima tu bukheri wa afya ,
Leo nataka tuangalie baadhi ya tabia za ajabu za team kiba kwa diamond

1) Team kiba wengi wanaongoza kwa kum follow diamond insta na huwa wanaongoza kutoa comments nyingi diamond akipost kitu

2)Team kiba wengi ni washabiki wa mdomoni kwa kuwa hata insta hawajam follow kipenzi chao kiba

3)Team kiba wengi wana pay attention kila diamond akitoa wimbo (audio au video )kuliko kiba akitoa video au audio

4)Team kiba wengi wanaongoza kuangalia you tube video za diamond kila zinapotoka wao wanakuwa wa kwanza kuzitafuta halafu cha ajabu zaidi wakimaliza kuangalia wanaziponda

5)Team kiba wanapenda kucheza au kuiga style za diamond za uchezaji kuliko za kiba mwenyewe na ukitaka kuona hili sana sana angalia club nyimbo zikipigwa watu wanacheza kimadoido kama ya diamond hata kama wimbo unaopigwa ni wa kiba

6)Ni rahisi team kiba kukosa show ya kiba kuliko kukosa show ya diamond

Ukitaka kuamini hilo subiri show ya diamond atakayopiga taifa "Diamond are forever". Lazima waende wengi na watatoa shangwe la kutosha lakini wakirudi nyumbani utasikia aaaah wapi diamond hana kitu chochote yule

7)Ikitokea msanii katoa wimbo mkali saana team kiba watamshindanisha huyo mtu na diamond na kusema kuwa huyo msanii kateka soko kwa sasa hamna wa kumfikia

Ukitaka kuamini hilo angalia darasa alipotoa wimbo wake wa mziki
Kwa nini walisema darasa kamfunika diamond na kwa sasa yeye ndiye kateka soko lote,

Hii inamaanisha mambo mawili
1. Mosi inamaana ya kuwa kabla ya hapo aliyekuwa ameliteka soko ni diamond na si kiba hivyo basi ujio wa darasa umempokonya ufalme diamond

2. Pili inamaana kuwa ili kiba alikuwa hafui dafu kwa diamond hivyo basi walikuwa wanatafuta mbadala wake wa kushindana na diamond

8)team kiba wengi hawajui ziara za show mbalimbali anazofanya kiba ,yani kwa lugha nyepesi hawajui kiba kwa sasa yupo wapi na anafanya nini

Lakini sasa waulize ratiba ya diamond watakutajia hata ya miezi mitatu ijayo watakwambia kwa sasa diamond yupo wapi na anatembelea gari gani

Waulize sasa kama wanajua kiba anatembelea gari gani na ananyumba wapi na wapi, hawajui lakin ukiwauliza diamond anakaa wapi haraka sana watakutajia madale

9)team kiba wanawajua mpaka watoto wa diamond lakini waulize wanamjua mtoto hata mmoja wa kiba uone maajabu ,ha ha ha ha

10)team kiba wanaifahamu sana familia ya diamond kuanzia mama yake,baba yake watoto wake,michepuko yake dada zake wa hiari nk geuza swali sasa waulize maswali hayo hayo kuhusu kiba uone maajabu hapo ,utafurahi na roho yako






Hapa ndipo utagundua wabongo wote ni team mondi ila ili kubalance mzani ndo kuna team kiba ambayo kiuhalisia haipo bali ni ya kufikirika tu


Tchaooooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…