Dogo G
JF-Expert Member
- Jul 6, 2018
- 1,052
- 440
Habari za wakati huu ndugu zanguni nyote katika jukwaa pendwa la jf,Siku hadi siku tunazidi kuongezeana maarifa kwa yale tuyajuayo ama tusiyoyajua.Leo nimeonelea niongelee suala moja ambalo wengi "huamini" lakini katika hiyo imani huenda kuna usahihi au kutokuwepo kwa usahihi.Na jambo ninalotaka kuongelea ni kuhusiana na majeshi ya ulinzi na usalama.
Kabla sijaenda mbali,Kiukweli kila jeshi/kikosi cha ulinzi kina umuhimu mkubwa sana katika usalama wa kila siku na yote katika yote hivyo vyombo vyote ni kumlinda na kufanya ulinzi na usalama wa raia.Hapa nimejumuisha na vyombo vidogo vidogo kama mgambo na taasisi zote za kiulinzi(makampuni binafsi ya ulinzi) ijapokuwa wengi huheshimu na kuuona umuhimu wa polisi,jwtz na magereza tuu wakijua ndio mihimili ya ulinzi(makosa),Msingi mkubwa wa ulinzi wako si Jeshi la wananchi,Polisi au Magereza bali ni kuanzia makampuni binafsi ya ulinzi ambayo hulinda sehemu mbalimbali kama vile katika masoko na ofisi mbalimbali za taasisi binafsi na za kiserikali ambako matukio mengi huanzia kwa hivyo tuvipe heshima vyombo vyote kwa nafasi yake.
Kwanza kabisa kabla sijaanza kudadavua haya majeshi yetu,tuelewe ni kwanini tunasema Polisi,Jwtz na magereza ni majeshi,je jeshi ni moja tuu hili ni miongoni mwa mambo ambayo wengine hufikiri kwasababu linaitwa jeshi la wananchi(hapana).JESHI ni kundi kubwa la askari waliopitia mafunzo ya awali ya kiuaskari/kijeshi(basic millitary trainings) ambapo huhusisha mbinu mbalimbali za kupambana na maadui/wahalifu pamoja na matumizi ya silaha mbalimbali.Pia MGAMBO,JKT na vilivyobakia si majeshi bali ni vitengo tuu au tunaita kamandi yaani vipo ndani ya hayo majeshi na hawana mafunzo kamili(mfano askari wa jkt) hawa ni kuruta tuu huweziwalinganisha na askari polisi jwtz au wa magereza kwahivyo huwezikumpeleka kwenye BATTLE FIELD(vitani au kukabiliana na wahalifu wakubwa) na ndio maana serikali inawaandaa hawa vijana ili waje kutumikia katika majeshi.Hivyo jkt si jeshi bali ni msingi wa kumuandaa kijana awe mwanajeshi,polisi au askari magereza na taasisi zingine za kiulinzi ila wapo chini ya jwtz.
Tanzania na dunia nzima kuna majeshi matatu ambayo ni Jeshi la wananchi kwa Tanzania(JWTZ),Jeshi la POLICE na JESHI LA MAGEREZA tuu.Sasa kuna mtu atahoji mbona hujajumuisha Zimamoto na uhamiaji?,Ipo hivi zimamoto na uhamiaji si majeshi bali ni idara za kutoa huduma na hivi ndivyo inavyofahamika hata kwa mataifa ya ulimwengu ulioendelea.Na kwa ulimwengu unaoendelea hivi vyombo huitwa SERVICES na sio FORCE.Hii ina maana kwamba zimamoto na migration hawajapitia Basic millitary trainings(mafunzo ya kijeshi ya awali) na ndio maana polisi huitwa FORCE ikimaanisha wamefuzu mafunzo ya kijeshi nadhani navyozungumzia mafunzo ya kijeshi askari wananielewa hapa.Vivyo hivyo pia kwa magereza nao wamepitia huo mzunguko na elewa kwamba mafunzo ya hivi vyombo ni UNIVERSAL yaani mafunzo ya JWTZ hapa nchini ni sawa na nchi nyingine zote DUNIANI isipokuwa kwa special force(ukomandoo tu kwani hawa mafunzo hutegemea pia uchumi wa nchi na mazingira.mfano huwezifananisha makomando wa Tanzania na Marekani) pia mafunzo ya POLICE nchini ni sawa na nchi nyingine zote duniani hivyo Askari wa chombo kimojawapo nchini anaweza kufanya kazi ya uaskari katika jeshi lolote kwa nchi yoyote duniani kwasababu zile taratibu za kimajukumu zinafanana isipokuwa lugha tu.
Lakini licha ya yote,hivi vyombo vimetofautiana kitu kimoja tuu ambacho wengi huchanganya.Kuna ULINZI(defence) na USALAMA(security) elewa hapo.Katika ulinzi wa taifa lolote duniani ulinzi hufanywa na JESHI LA WANANCHI(defence forces) wakati usalama wa nchi yoyote hufanywa na POLICE pamoja na MAGEREZA lakini usalama wa ndani hususani hufanywa na polisi.
Sasa kuna mtu atahoji tofauti ya ulinzi na usalama ni nini!,Ipo hivi tunaposema ulinzi katika kupambana na adui au mhalifu huhusisha mambo mawili KUUA au KUKAMATA kwa hivyo kumbe jeshi lolote linaweza kuua au kukamata kulingana na malengo na hii ni kwa mujibu wa sheria za nchi na ndio maana wengi tunajua kuwa kazi ya jeshi ni Kuua basi.Lakini USALAMA ina maana unapopambana na adui/mhalifu ni kukamata tuu hii ni kwa mujibu wa sheria na ndio maana askari polisi anaweza kupambana na jambazi akamtaiti na kumkamata ili kumpeleka kwenye vyombo vya sheria ijapokuwa tunafahamu askari wetu nao mwendokasi sana kati ya mpambano na majambazi kumi eti nane lazima risasi iwalenge vibaya na wanafariki wakiwa njiani kuelekea hospitali (nadhani ni technique ya kuyamaliza tuu) Na jwtz,Polisi na magereza ni vyombo vya mama mmoja ila baba tofauti na vinategemeana.Mafunzo yao yanafanana kwa 3/4 isipokuwa kwa sehemu ndogo tuu,Leo hii utaona kama JWTZ ni zaidi ya polisi si kweli ila ni utofauti wa kimajukumu tuu kwani inawezekana leo katiba ikabadilishwa polisi wahusike na ulinzi(mipaka) na jwtz wakahusika nausalama(ulinzi wa ndani) na mkawadisi vile vile kwan kuishi na binadamu kazi.
Na jambo jingine kuhusu hivi vyombo ni kuwa vyote vipo chini ya serikali na viliaanzishwa ili kurahisisha michakato ya serikali kwa minajili ya kutii mamlaka za serikali kwa mujibu sheria.Lakini tunaona the way serikali inavyokuja kuvitumia vice versa(siasa sumu) hivyo kuonekana kama vipo kwa maslahi zaidi ya kiserikali.
Kwa leo niishie hapa panapo maajaaliwa nitaelezea kuhusiana na vikosi vya haya majeshi na Usalama wa taifa, kwa hoja na maswali yoyote karibuni.