UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,710
- 12,784
Nsikuchoshe na usinchoshe,Tusichoshane!
Kwa namna Hali inavyoendelea Kuwa mbaya katika jamii hasa mambo wanayoyafanya hao mabinti wanaoitwa "wadada wa kazi" nimeona na Mimi angalau nikatoa ushauri Kwa jamii hasa hao waajili "Mabosi" Ili kama kutakuwa na hatua za kuchukua zichukuliwe ili kuilinda jamii hasa watoto!
Jambo kubwa linaloitesa jamii ya watanzania ni "ULIMBUKENI"
Hivi kweli kabisa mwanamke ambaye unaye mtoto mmoja tu na muda unashinda nyumbani unaenda kuajili dada wa kazi wa kazi gani? Kwamba,huyo mwanao amekushinda kulea? Kwamba kufua nguo zako,za mwanao na mumeo zimekushinda? Kwamba kupika chakula chako,mwanao na mumeo kumekushinda? Kama mwanao wa kumzaa amekushinda kulea hadi utafute dada wa kazi akulele basi hupaswi kuitwa mwanamke au mke,bila shaka utakuwa na matatizo ya kiakili!
Umepanga kachumba kamoja na sebule wewe naye kutwa kusumbua watu wakutafutie binti wa kazi,hivi Kwa kazi gani hasa zinazokushinda wewe na mwanao kwenye vyumba viwili hivyo? Kama si ULIMBUKENI ni nini?
Unakuta familia Ina watoto wakubwa tu wakiwemo Vijana na mabinti,lakini kwasababu za ULIMBUKENI wanaona wakiwaambia watoto wao wafanye kazi za nyumbani ni kuwasumbua na uzungu mwingi,unakuta mitoto hiyo kufanya kazi za hapo nyumbani ikiwemo kuwaangalia wadogo zao haiwezi hadi waajili mabinti wa kazi, kiukweli kama hapa JF ipo hiyo familia wewe mama au baba inapaswa ujitafakari!
Wenzetu huko Ulaya na Marekani huwa wanaajili wamama & wababa wa kazi ambao ni watu wazima wenye akili timamu pia wanaajili kwasababu wenzetu Wana makasri makubwa ambayo yanahitaji usaidizi!
Wewe mswahili mwenzangu kutoka hapo nyanchabhakenye au hapo Ikwiriri mwenye ka nyumba ka vyumba viwili nawe unataka mfanyakazi,hivi Kwa kazi gani hasa? Kibaya zaidi mnaajili katoto kadogo ambako Nako bado kanahitaji malezi eti ndo kakulelee mwanao,hivi tuko serious kweli kama jamii?
Kwanini kama tunataka wasaidizi wa ndani tusiajili watu wazima? Mtu mzima mwenye akili timamu hata mtoto akijinyea atajua ni mtoto tu, na ataenda kumnawisha na kumbadilisha nguo, lakini hivi vitoto mnavyoajili mtoto akijinyea katajua mtoto anafanya kusudi na kataanza kumpiga makofi kakidhani huyo mtoto ni mtu mzima!
Bila aibu unakuta jitu Zima limetunisha mgongo kama chura pale sebuleni au kibarazani linapiga simu Mwanza,Iringa au Singida likitaka binti wa kazi tena linasisitiza kabisa "Nitafutieni ambaye ni mdogo mdogo nitamfunza mwenyewe,hao watu wazima siwataki wataniharibia nyumba", Seriously?
Yaani uajili katoto ambako kanafaa kawe shule na watoto wenzie halafu ndiyo utegemee kakuangalizie mwanao?
Watoto wenu wataendelea kuuawa na kuteswa kama msipobadilika!
Kama unahitaji msaidizi wa kazi ajili mtu mzima mwenye akili timamu ambaye unajua kabisa hata ukiwa kazini mwanao atakuwa kwenye mikono salama, siyo unaajili katoto kadogo au teenager ambaye bado mwili wake unachemka, ndiyo unakuta anamuacha mwanao ndani yeye anakipeleka!
SULUHISHO
Ajili mtu mzima wa makamo akuangalizie wanao,achana na habari za teenagers Hawa bado ni watoto na watakusumbua kama si kukutesea watoto!
Kama huna haja na msaidizi wa kazi acha mara moja,usifuate mkumbo tu wa kimazoea!
Pia unapoajili mtu mzima uwe tayari kumlipa vizuri,siyo unaajili mtu halafu mwisho wa Mwezi unamlipa Tsh 60,000 hili haliwezekani!