proxy
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 1,477
- 1,346
Wadau hawa idara ya Maji ya Songea ni jipu linalosubili kutumbuliwa ,nimeomba kuunganishwa Maji taklibanj mwezi sasa kila nikienda wananiambia bado vifaa hamna vya kuunganishiwa Maji,ilihali nimeshalipa kila kitu mpaka gharama ya mchimba mtaro,sasa ninachojiuliza hivi sababu zingine za kusema vifaa hamna zinatoka wapi,wakati mteja ameshalipishwa kila kitu? Na kama kweli vifaa hamna kwa nini mteja anakuja anaambili wakati ameshalipa kila kitu wakati kabla hajalipa mmemwambia kila kitu kipo store? ,Hivi kwa design hii hamuoni kwamba nyinyi ni kikwazo cha kukwamisha nia ya mheshimiwa ya kuisogeza nchi kwenye uchumi wa kati? ,Na mnajua gharama ya mteja kukosa Maji kwa muda wote huo ili hali kashalipia kila kitu?. Hayo mambo ni yakizamani sana kama hamjui.Acheni hizo bwana.