Hawa Hamas wanaopigana dhidi ya Israeli ni kina nani hasa?

Raphael Mtui

Member
Nov 26, 2024
68
190
Tupate elimu kidogo wana JF: Hamas ni chama cha siasa ambacho kinatawala ukanda wa Gaza. Ingawa ni chama, lakini pia Hamas ni kundi la wanamgambo wenye silaha mfano wa jeshi.

Hamas ni ufupisho wa maneno Harakat al-Muqawama al-Islamiyya ambapo kwa Kiswahili ni Vuguguvu la Upinzani la Kiislamu (Islamic Resistance Movement).

Katika vyama vyote vya kisiasa vya Wapalestina, hiki ndio chama kinachojiweza kuliko vyama vyote kutokana na kufadhiliwa kwingi na wale wanaounga mkono harakati zao.

Hamas hupokea misaada mikubwa kutoka nchi kama Iran, Qatar na Uturuki. Misaada hiyo ni pamoja mabilioni ya fedha, na nguvu za kijeshi kama kupewa silaha, na mafunzo ya kijeshi.

Moja ya njia nzuri za kuielezea Hamas ni jinsi walivyo na nia na juhudi nyingi za kuifuta Israeli duniani.

Yaani, sababu kuu za uwepo wao duniani ni kuhakikisha wanaifuta Israeli, na kisha wajenge taifa la Kipalestina wakishaondoa Israeli katika ramani ya dunia!

Wao wakilala-wakiamka, ajenda yao kuu ni kuangamiza Israeli.

Ni kundi ambalo limekuwa halipumziki katika kuishambulia Israeli. Iwe kuna vita rasmi au hakuna, ni kawaida tu Hamas kuvurumisha rockets kutoka Gaza kuelekea Israeli.

Sasa tukumbushane kitu:

Unaposikia Wapalestina, fahamu kwamba wako katika maeneo mawili: Wapalestina wa ukanda wa Gaza na Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi (West Bank).

Uadui kati ya Wapalestina na Waisraeli ni mkubwa mno, ndipo ikabidi kutokee kutengana huko. Mwanzoni walikuwa wakiishi pamoja ndani ya nchi moja ya Israeli.

Yakatengwa maeneo mawili kwa ajili ya Wapalestina, Gaza na West Bank.

Jenga picha kwa mfano nchi yetu Tanzania:

Ni sawa na useme eneo lote la Mkoa wa Pwani ndio West Bank na pale wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ndio Gaza.

Kingine cha kujua haraka ni kwamba, Wapalestina waishio Gaza na wale waishio West Bank hawapendani kabisa. Wala hawaelewani. Kila kundi lina misimamo na itikadi zake.

Lakini ndani yake kuna mambo mengi yasiyoeleweka bayana, ila kwa ufupi wanachukiana kweli kweli!

Ndio maana, hujawahi kusikia Wapalestina wa Gaza wakishirikiana na West Bank kumpiga adui yao Israeli.

Hata vita vilivyoanza tarehe 7 Oct 2023 huwezi kuona Wapalestina wa West Bank wakishirikiana kuipiga Israeli.

Utaona tu Hezbollah kutoka nchini Lebanoni wakishirikiana na Hamas, hata nchi kubwa kama Irani ikiingilia na kushambulia Israeli moja kwa moja.

Lakini sio Wapalestina waishio West Bank. Na hiyo haimaanishi kwamba Wapalestina wa West Bank sio maadui wa Israeli.

Sasa kumbuka tena hili:

Serikali rasmi inayotambulika duniani kuwa serikali ya Wapalestina ni ile ya West Bank. Wote tunafahamu kile kitu kiitwacho Mamlaka ya Wapalestina (Palestinian Authority). Palestina haijawahi kutambulika kama nchi duniani, lakini wametambulika tu kama 'Permanent Observer'.

West Bank haiitwi nchi, na Gaza ndio kabisa haiwezi kuitwa 'nchi'.

Lakini angalao West Bank ina serikali rasmi ya Wapalestina, na mji wao mkuu ni Ramallah hapo ndani ya West Bank.

West Bank ina eneo kubwa maradufu ukilinganisha na Gaza.

Tuache hayo:

Hamas ni chama kilichoundwa mwaka 1987 katikati ya ile intifada ya kwanza.

Kuanzia mwaka 2007, chama hiki kilipofanikiwa kuondoa Mamlaka ya Palestina kwenye uongozi kwa kushinda chama cha Fatah, hakika wao ndio wamekuja kuwa ndio serikali ya Gaza na wakatamalaki kweli kweli!

Wamekuwa 'mabeberu' wasioshikika na Wapalestina wenzao wa West Bank.

Miaka kumi baadaye, yaani mwaka 2017, Hamas ilibadilisha itikadi yake na kusema haiwazi kuifuta Israeli duniani. Lakini hata hivyo, hadi sasa (2024) hawajawahi kuitambua Israeli kama nchi, na imeendelea na harakati zile zile za kuishambulia Israeli.

Raphael Mtui 0762731869
 
Back
Top Bottom