Hatua za kukabiliana na msongo wa mawazo unaotokana na migogoro ya kifamilia

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
16,464
35,600
Msongo wa mawazo ni hali ya mfadhaiko wa kiakili ambao hujitokeza ghafla pale ambapo mtu anapokuwa na shida, tatizo,au kikwazo chochote ambacho hana uwezo wa kukabiliana nacho.Uwezo wa kukabiliana na kikwazo hicho unaweza kuwa uwezo wa kifedha, kiafya, kielimu,nguvu ya mwili katika kukabiliana nacho.

VIFUATAVYO NI VIASHIRIA VYA MSONGO WA MAWAZO
Msongo wa mawazo huwa na viashiria vifuatavyo
#Moyo kwenda mbio, miguu kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kichefuchefu, kuchanganyikiwa, hasira kupita kiasi, kupoteza hisia za mapenzi, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu, kujuta, kutamani kujiua au kumdhuru mwenza au mzazi

#Tumbo kuvurugika au kutetemeka sana, kujiona upo hatarini muda wote,kuhisi unataka kurukwa akili, kuhisi unataka kudondoka ghafla,kuanza kulia, kujitenga,kukosa nguvu za kutoka kitandani au kulala sana mpaka unachoka,

#kukosa hamasa ya kufanya kazi,kukosa maamuzi,kukata tamaa ya maisha,kujiona mzee sana kabla ya umri,kukonda sana ghafla au kunenepa sana ghafla.

#Kula sana vyakula bila mpangilio au kukosa hamu ya kula,kukosa usingizi au kulala mpaka unachoka,kuweweseka sana,vidole kufa ganzi, kuumia kooni, kupaniki,kubanwa na choo ghafla.

VIFUATAVYO NI VYANZO VYA MSONGO WA MAWAZO UNAOTOKANA NA MATATIZO/MIGOGORO YA KIFAMILIA
Vyanzo vyake vipo katika makundi mawili
I.MAHUSIANO YAKO NA WAZAZI WAKO
Hapa unaweza kuzongwa na mawazo sana kwa sababu zifuatazo
#mzazi au wazazi wako wote wawili kusumbuliwa na matatizo ya kiafya kama vile ugonjwa wa akili,kuugua mara kwa mara, kuugua muda mrefu sana bila kupata nafuu,uzee (umri mkubwa sana), kusumbuliwa na maumivu makali sana ya mifupa pamoja na kuumwa kichwa na mgongo, ulemavu wa kudumu.

#mzazi au wazazi wako wote wawili kuwa na tabia sugu /uraibu (addiction) wa ulevi kupindukia, kucheza kamari, uhalifu wa silaha,wizi, kushiriki mapenzi na watoto wadogo kama housegirl au wanafunzi,kutumia fedha nyingi sana bila hesabu,kupenda sana starehe,kupenda sana sifa,kuishi maisha ya kifahari sana kuliko uwezo wa familia, kujihusisha na imani za kishirikina,kuwa na tabia zenye kukudhalilisha mtaani.

#mzazi au mzazi wote wawili kuonekana na hasira kupita kiasi,lawama, matusi, vitisho,tabia ya ubabe na ukosoaji kupita kiasi, kukugombeza sana,kukuchafua hadharani,

#mzazi au wazazi kwa pamoja kulalamika sana kuwa wapo na upweke na kudai unawapuuza,hauwajali tangu umeoa au kuolewa na kila juhudi za kujiweka karibu nao zinaonekana kuibua ugomvi zaidi kuliko suluhu.

#Kuona wazazi wanaingia kwenye ugomvi kila siku mbele yako unaona wanatupiana lawama, matusi, vitisho,kashfa na tuhuma za usaliti na ushirikina.

#Kuona kila siku mzazi au wazazi wako wote wawili wanakufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina yenye udhalilishaji, kusambaza umbea, kuzusha uongo,kukataa zawadi zako,kukaa kimya bila mawasiliano yoyote kila ukitaka kujieleza au kujenga ukaribu nao

#kuona mzazi au wazazi wanafanya upendeleo kwa makusudi kwa baadhi ya ndugu zako n.k

#kuona mzazi au wazazi wako wote wawili wakimchukia na kumpiga vita mwenza wako mara kwa mara na kukulazimisha muachane bila sababu zozote za msingi

#Kuona ndugu zako wanataka kupigana ngumi na wazazi wako kwa sababu ya mali

#mzazi au wazazi wako kukulazimisha utoe /uchangie fedha nyingi sana kuliko uwezo wako,kuona ndugu zako wa damu wanadai wewe si ndugu yao wa damu na kutaka ujiondoe kwenye familia husika.

#mzazi/wazazi wako wote kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia mwenza wako kila siku ukiwa kazini na kugeuza kibao kila ukirejea nyumbani

II.MAHUSIANO YAKO NA MWENZA WAKO
Kwa upande wa mahusiano baina yako na mwenza wako unaweza kupatwa na msongo wa mawazo kwa sababu zifuatazo
#Mwenza wako kuibua ugomvi kila siku ili apate kisingizio cha kuondoka nyumbani kwako aende kwa wazazi wake
#mwenza wako kuwafokea , kuwatukana, kuwadhalilisha wazazi wako kila siku ukiwa kazini kisha anageuza kibao kwao kila ukirejea nyumbani

#mwenza wako kukubambikia kesi mahakamani,mwenza wako kuzaa na mtu mwengine kisha anataka kuleta mtoto ndani ya familia,mwenza wako kugoma kukupa unyumba kila siku na kuibua ugomvi kila siku ukitaka kumgusa.

#mwenza wako kukulazimisha ubadilishe hati miliki za mali zako uandike majina yake kama hauwezi muachane

#mwenza wako kukuomba fedha nyingi sana ghafla na kutishia muachane kama utashindwa kumpatia fedha hizo.

#mwenza wako kuuza mali zako zote kisha kutokomea kusikojulikana

#mwenza wako kukufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina ya udhalilishaji,kuzusha uongo juu yako,kukopa fedha nyingi sana kwa dhamana ya mali zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…