Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,410
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wamekuwa wanasumbuka na fedha kwa maisha yao yote.
Tangu wanaingia kwenye umri wa kufanya kazi, wanafanya kazi kila siku na kwa maisha yao yote.
Lakini kwa bahati mbaya sana, bado wanakuwa hawafikii hatua ya kuweza kuishi aina ya maisha wanayokuwa wanayataka.
Hata wale ambao wanakuwa wameajiriwa na wanapostaafu kupewa mafao yao, bado yamekuwa hayawatoshelezi kuendesha aina ya maisha wanayotaka.
Yaani kwenye ajira, kustaafu imekuwa inachukuliwa kama hatua ya mtu kuanza kufanya shughuli za kuingiza kipato. Wakati dhana nzima ya kustaafu ni mtu uweze kuendesha maisha yako bila ya kutegemea kipato cha moja kwa moja.
Kila mtu ambaye anafanya kazi yoyote ya kuingiza kipato, anayo fursa ya kufikia uhuru wa kifedha. Wengi wanashindwa hilo kwa sababu hawapati miongozo sahihi.
Mwandishi Chris Hogan kwenye kitabu chake kinachoitwa EVERYDAY MILLIONAIRES ameonyesha jinsi watu wa kawaida kabisa walivyoweza kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yao na jinsi hata wewe unaweza kufanya hivyo.
Kitabu hicho ni matokeo ya utafiti uliofanywa kwa mamilionea zaidi ya elfu 10 na kuweza kupata taarifa nyingi sana kuwahusu. Utafiti huo uligusa kila eneo la matajiri, kuanzia mitazamo, fikra, shughuli wanazofanya, mahusiano, familia n.k.
Kupitia kitabu hicho, mwandishi anatupa hatua za mtu yeyote kuweza kuzitumia kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yake. Karibu ujifunze hapa, ukachukue hatua na kujijengea uhuru wa kifedha.
SURA YA 11; CHUKUA HATUA KUJENGA UHURU WA KIFEDHA.
Watu wengi huwa wanafikiria uhuru wa kifedha ni kitu kigumu sana kwa watu wa kawaida kuweza kufikia. Huwa wanadhani ni mpaka mtu awe na utajiri wa kiasi fulani ndiyo anakuwa huru kifedha.
Lakini hilo siyo kweli, uhuru wa kifedha unamaanisha vitu vikubwa vitatu;
Moja ni unakuwa huna deni lolote, yaani hakuna mtu yeyote anayekudai kitu chochote.
Mbili ni unakuwa na uwekezaji ambao unakua thamani na kumfanya mtu kuwa na utajiri.
Tatu ni unakuwa na kipato endelevu maisha yako yote, ambacho kinaingia hata kama mtu hufanyi kazi moja kwa moja.
Unaona hapo rafiki, huhitaji manamba makubwa sana kuwa na uhuru wa kifedha, ni kuzingatia hayo matatu na kwenda vizuri.
Faida za uhuru wa kifedha.
Uhuru wa kifedha una manufaa makubwa sana kwa kila anayefikia. Kwa sababu uhuru wa kifedha unakuweka huru kwenye maeneo haya manne;
1. Uhuru wa muda; unakuwa huru kutumia muda wako vile unavyotaka wewe mwenyewe.
2. Uhuru wa kipato; hupangiwi na mtu yeyote uingize kipato gani.
3. Uhuru wa machaguo; unakuwa huru kuchagua chochote unachotaka.
4. Uhuru wa upatikanaji; unaweza kupatikana kwa watu wako wa karibu pale wanapokuhitaji.
SOMA; Weka Kazi Na Kuwa Na Msimamo Kujenga Utajiri Mkubwa.
Hatua za kufikia uhuru wa kifedha.
Ili kufikia uhuru wa kifedha, mtu unapaswa kufanya yafuatayo;
1. Fanya uwekezaji wa muda mrefu, fikiria kwa miongo na siyo miezi.
2. Jenga utajiri wako taratibu, epuka njia za mkato za kujenga utajiri, utapoteza zaidi.
3. Lipa madeni yako yote, madeni ni kaburi linalozika umasikini.
4. Ishi chini ya kipato chako, akiba ndiyo mbegu ya utajiri.
5. Pata elimu ya kawaida, usitumie gharama nyingi au madeni kwenye kupata elimu.
6. Wajibika na maisha yako, usimlaumu yeyote.
7. Weka na fikia malengo yako, malengo ndiyo yanayokuongoza.
8. Fanya kazi kwa juhudi kubwa sana, kazi ndiyo msingi mkuu.
9. Pata ushauri kutoka kwa watu sahihi, wataalamu kwenye eneo la fedha.
10. Acha jina na sifa nzuri.
11. Toa msaada kwa wenye uhitaji.
Hapa tumejifunza hatua za kuchukua ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yako. Karibu upate UCHAMBUZI KAMILI wa kitabu hiki cha EVERYDAY MILLIONAIRES kwa kubonyeza MAANDISHI HAYA.
Tumekuwa na mjadala mzuri wa uchambuzi wa kitabu hiki cha EVERYDAY MILLIONAIRE ambapo watu wameshirikisha yale waliyojifunza na hatua wanazochukua. Fungua hapo chini kujifunza zaidi kutoka kwenye kitabu na michango ya wengine.
View: https://youtu.be/K-Qlw3QAKsE
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
www.amkamtanzania.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.