tzhosts
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 398
- 503
Habari za wakati huu;
Leo nataka nilete darasa fupi la jinsi ya kutengeneza website (Tovuti ) kwa ajili ya biashara yako kwa gharama nafuu kabisa.Nitaanza kwa kuelezea kidgo tovuti ni nini na kazi yake ni nini?
Tovuti ni nini?
Tovuti ni anuani ya mtandaoni.Ni sehemu katika mtandao ambamo unaweza kuweka taarifa zako ili ziwafikie watu wengi kwa urahisi.Tovuti ni zana ya kufanyia masoko na inaweza pia kuwa zana ya mauzo na zana ya kusimamia biashara yako.Katika zama hizi kumiliki tovuti ni muhimu sana katika kuendesha biashara .
Hatua zifuatazo zinahusika katika kuanzisha na kuendesha tovuti
1. Hatua ya kwanza ni kuchagua jina la tovuti(Domain name)
Katika hatu hii unachagua jina ambalo ni rahisi kukumbuka,linaakisii biashara yako.linavutia.Unaweza kuchagua jina linalokufaa kupitia link hii:
Domain Registration - Search and Buy Domain
2. Kuandaa maudhui ya tovuti(Content/Profile)
Maudhui yako yahusisha taarifa zote muhimu kuhusu biashara yako ili kumwezesha msomaji kuelewa kwa kina malengo,shughuli na uwezo wako kibiashara.Hapa unaweza kutafuta mtaalamu wa kuandika maudhui/copywriter ili akuandalie muadhui ya kuvutia wateja.
3. Kuandaa mpangilio wa maudhui(Layout/structure)
Mpangilio wa maudhui yako uwe rahisi kufikiwa na kusomwa na watu pamoja na robots za mtandaoni.Mpangilio uoneshe kwamba wewe ni serious business na unalenga kutoa huduma bora kwa wateja wako wote.Hapa unaweza kutafuta mtaalamu wa kutengeneza mwonekano wa tovuti yako au unaweza kutafuta mionekano(templates ) ambazo zinaweza kufanyiwa marekebisho.WordPress inakuwa na uwezo zaidi kwa sababu ya idadi kubwa ya watumiaji.
4. Kuweka maudhui yako mtandaoni(Hosting)
Tafuta hosting agent ambaye ana uzoefu,na anakupa thamani halisi ya pesa yako bila kuathiri ubora.Unaweza kupata packages za kuhost ambazo zinaendana na budget yako kupitia link hii.
Linux Shared Hosting
Linux Hosting Plans: Cheap Linux Web Hosting Plans for Domain Name Hosting, Domain Name Web Hosting, Web Domain Hosting, PHP Hosting at our website.
tzhosts.com
5. Kusambaza maudhui yako mtandaoni
Hakikisha unatumia mbinu mbalimbali za kusambaza maudhui yako ikiwamo mitandao ya kijamii na search engines ili kuwafikia watu wengi Zaidi
6. Kufuatilia utendaji wa tovuti yako
Fuatilia utendaji wa tovuti yako kwa kuhakikisha kwamba unaangalia idadi ya watembeleaji,wanakotekea na matokeo unayopta ili kuhakikisha kwamba unakuwa na takwimu sahihi kuhusu tovuti yako.
Iwapo ungependa kufahamu zaidi kuhusu uanzishaji na uendeshaji wa tovuti tafadhali wasiliana nasi kwa email:info@tzhosts.com