Shambani kwangu nimepakana na Mjumbe,huyu bwana na mke wake wamekuwa wakiwalaghai wafanyakazi wangu kila Mara ninapopata mfanyakazi mpya na kupelekea wao kuondoka,na kuna taarifa pia wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi kuniibia vyakula vya mifugo na mifugo yenyewe,yupo mfanyakazi nilimfukuza siku za nyuma na wao wamemwita wanaishi naye ambapo kila MTU anashangaa kwani hawana Kazi za kiasi cha kuajiri mfanyakazi,naomba ushauri niwachukulie hatua gani watu hawa?