Mlizoea kuutumia udhaifu wa serikali kama mtaji wakisiasa sasa ile nafasi haipo.Tatizo linapotatuliwa UKAWA kwenu ni kero.
Badilikeni vinginevyo mtapotea!
Hekima ni kumuelewesha asiyejua sio kugombana naye...!!! iko hivi
Mwanzoni kabisa wakati tunaingia kwenye ulimwengu wa digital ving'amuzi vilikuwa juu sana kuna baadhi vilifika mpaka 250,000/=.hii ni kwakuwa wasambazaji hawakuwa wengi na kodi zilikuwa nyingi hapa Naongelea miaka ya 2000+
Baadae wakaja wasambazaji wengi kipindi cha Kikwete hivyo demand ikawa na supply vikaenda sambamba, ikawa kuna variaties na kushindanisha kwenye ubora na bei
Wananchi walikuja kulalamika ughali wa bundle za mwezi au airtime au vifurushi... .kwahiyo yakafanyika makubaliano kuwa serikali iondoe baadhi ya kodi ili
1.bei za ving'amuzi zipungue
2. Kuwepo na unafuu wa vifurushi na local channels zionyeshwe bure
Tangu hapo kumekuwa na figisu nyingi kwakuwa ukionyesha local channels bure mapato yanashuka huku unalipia masafa
Hivyo basi kinachofanyika kwasasa ni kucheza na bei za ving'amuzi na vifurushi vya mwezi ili supplier asipate hasara lakini bado aendelee kutoa huduma
Nimechukua muda kukuelewesha kwa faida ya wengi