Hatimaye nimeanza rasmi kilimo cha miti ya mbao Iringa

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,597
Baada ya kuona fursa hii kupitia jukwaa hili nimeamua kuifanyia kazi.
Mwaka huu mwezi wa 8 nikasafiri kuja Iringa mji wa Mafinga nikafanya research na kugundua kweli kilimo hiki kinafanyika na mashamba yanapatikana!
Nikafanikiwa kupata Shamba ekari 5 maendeo ya Ifunda kwa 250,000@ garama za resekali ya kijiji ni 50,000. Kusafisha shamba ikanigharimu 150,000 maana lilikuwa na vichaka.
mwezi huu wa 12 nimefanikiwa kupanda ekari zote miche ya pine kwa gharama zifuatazo. Miche 2250 @sh 100(miche 450 kwa ekari 1) Gharama za wapandaji ni sh 60 kwa kila shimo moja. Mwakani Mungu akipenda Nina lengo la kupanda miche ya milingoti ambayo inawahi kuvunwa kabla ya pine.

Hii ni fursa nzuri kwa wale wenye malengo ya muda mrefu. karibuni
 
Hongera ndugu yangu....nilikuwa mkoa wa Iringa na Njombe mwezi December kikazi, nilipata wasaa wa kuongea na wenyeji wangu. Hakika nimejifunza mengi. Niliambiwa kuna kitongoji chaitwa Mapanda karibu na Mafinga mashamba yanapatikana kwa unafuu zaidi. Njombe nako ni hivyo hivyo. Panapo majaliwa nitakuwa huko Mwanzoni mwa February 2017 nami angalau nimiliki eka 5 kwa kuanzi
 
Hongera

Mimi ni Afisa miti aka Afisa misitu, kama ukitaka ushauri wa kitaalamu tuwasiliane. Nitakusaidia zaidi namna ya kufanya TENDING and SILVICULTURAL OPERATIONS.

Karibu
 
ni biashara nzuri sana!!!! mapanda ipo almost 70km kutoka Mafinga japo mashamba ni bei rahisi
 
Kidadari..
Nahisi utakuwa mwenyeji sana maeneo hayo, miundombinu yake ikoje, bei ya shamba jipya?
 
Mimi nipo kigoma lakini nahitaji kufanya kilimo cha miti, naomba ushauri huku kigoma kilimo cha miti kimawezekana? na ni miti gani
 
hongera sana mkuu,unatupa nguvu wengine kujongea huko.nitaomba muongozo muda ukifika.nakusanya taarifa kwanza.
 
Hongera

Mimi ni Afisa miti aka Afisa misitu, kama ukitaka ushauri wa kitaalamu tuwasiliane. Nitakusaidia zaidi namna ya kufanya TENDING and SILVICULTURAL OPERATIONS.

Karibu
Mkuu ndo nini ebu toa shule tujue mana waweza kuta watu wanahitaji ila hawajui inaitwa ivo
 
Rafiki nami nko na plans hiyo ya shamba la miti nipe namba yako kwa mawasiliano
 
Mkuu nipe ufafanuzi.mfano umenunua shamba ukapanda miti.ikivuna bado itakuwa mali yako au ukivuna ndio basi tena
 
Hongera sana mkuu,

Mimi nakusanya nguvu kwanza nina shamba kama la hekari 25 lipo huko mkoani songea.

Lote nitaliweka miti
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…