BabuKijiko

Member
May 3, 2024
24
37
Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio cha Wastaafu na hivyo imepandisha Malipo ya Mkupuo kutoka 33% hadi 40%

Pia, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameagiza kuongezwa kwa malipo hayo kwa Wastaafu waliokuwa wakilipwa 25% sasa watalipwa 35% katika Mwaka huu wa Fedha


====

Pia soma: LIVE - Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, leo Juni 13, 2024 Bungeni, Dodoma
 
Kwa nini mtu asilipwe hela yake yote? Mtu kafanya kazi kwa asilimia 100 kwa nini alipwe asilimia 30 ya mafao yake? Kwa nini wabunge wao wanachukua mzigo wote hamuwawekei hiyo pesa? Hiyo asilimia inayobaki kwenu ndio mnaichezea kwa safari zisizo za lazima. Hebu hili lifike mwisho sasa. MTU CHAKE APEWE!
 
Akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio cha Wastaafu na hivyo imepandisha Malipo ya Mkupuo kutoka 33% hadi 40%

Pia, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameagiza kuongezwa kwa malipo hayo kwa Wastaafu waliokuwa wakilipwa 25% sasa watalipwa 35% katika Mwaka huu wa Fedha
View attachment 3016524
Hii 40% (malipo ya mkupuo ya kiinua mgongo) bado haitoshi, serikali haijasikia bado, msitudanganye

Tunataka kikokotoo cha awali kabla hiki cha 33% kuanza kutumika.

Serikali iache wizi mara moja kuibia wastaafu fedha zao. Wabunge kama mnajipenda kwenye hili, kataeni pendekezo hili la serikali. Wastaafu Tunataka kikokotoo cha 50%. Otherwise tutajiunga na CHADEMA kuuwasha moto wa kuwakataa.!!

Serikali iache wizi wa kuiba kupitia kwa wastaafu na kufanyia anasa pesa zao!

Lipeni madeni ya Trl 4.6 mlizokopa kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii Ili wastaafu tulipwe malipo stahiki ya kiinua mgongo cha 50% kama awali kabla hamjaanza kuchota fedha za mifuko hii!!
 
Kupitia bajeti, Rais Samia Suluhu ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliyopo sasa hadi asilimia 40. Mabadiliko haya yatawagusa kundi kubwa la watumishi wa umma wakiwepo Walimu, kada ya afya, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na makundi mengine yaliyopo Serikali kuu na Serikali za Mitaa.

Pia Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33 sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa huu wa fedha.

Serikali imesema itaendelea kuangalia maslahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko.
 
Kwanini wasiweke 50-50!
Monthly pension itashuka sana waulize wastaafu waliolipwa mkupuo asilimia 25 wanaishi maisha ya Raha sana pension ya Kila mwezi hawapishani sana na walioko ofisini sababu monthly pension ni kama 75 percent ya mshahara walikuwa wanapata

Ukiweka asilimia 50 maana yake unataka monthly pension Yako iwe nusu ya mshahara uliokuwa Ukipata kazini haiko vizuri Kwa mstaafu

Binafsi ningepekeza wastaafu walipwe asilimia kumi tu mkupuo ili monthly pension Yao iwe asilimia 90 ya mshahara waliokuwa wakipata kazini

Lakini mtoto akililia wembe mpe ndicho serikalli imefanya
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Hivi hiyo monthly payment huwa inategemea vigezo gani? Kwa mwalimu anaweza kupata ngapi kwa makario eg kama atalipwa 40% kwa mkupuo.
 
Warudishe tu kile kikokotoo cha zamani. Wastaafu wanataka mpunga wa kueleweka ili wafanyie mambo yao ya msingi mara tu baada ya kustaafu.
Kama huelewi 50 50 tukueleweshe Kwa lugha Rahisi maana yake unachukua 50 percent mkupuo na monthly pension utalipwa 50 percent ya mshahara ulikuwa unapata maisha Yako yote

Ukitaka 80 percent mkupuo ina maana utalipwa monthly pension 20 percent ya mshahara wako maisha Yako yote kitu ambacho Sio Afya sana Kwa mstaafu
 
Monthly pension itashuka sema waliobeza kikokotoo hawajielewi kuwa kadri unavyochukua Hela ya mkupuo kubwa monthly pension inashuka na Maisha ni monthly pension sio Hela ya mkupuo

Hela ya mkupuo hukata upesi
Kuna mwalimu mmoja alichukuwa hii ya mkupuo, akakimbilia kujenga kijijini anakoishi, akagaiwa watoto kidogo na iliyobaki akawa ananywea pombe mpaka ikakata. Sasa hivi anaishi kimaskini kweli kweli. Nadhani huyo angepata hii ya kila mwezi ingemsaidia zaidi.
 
Back
Top Bottom