Hatimaye FRELIMO iko matatani, mwisho wake umefika!

nyonyodawa

Member
Nov 11, 2024
42
133
Kwa wanaofuatilia siasa za Mozambique, hali ni mbaya kwa chama tawala cha Frelimo pamoja na serikali iliyoko madarakani. Baada ya uchaguzi kuisha na serikali kujitangaza kushinda kwa wastani wa asilimia sabini, wananchi wameikata, wakiongozwa na kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane.

Kinachotokea sasa hivi ni kwamba huyu kiongozi wa upinzani ndiye mwenye nguvu na sauti kuliko serikali; yeye ndiye anayeamuru nini kifanyike. Anaratibu maandamano akiwa mafichoni, baada ya kukimbia nchi kufuatia mauaji ya wakili wake.

Hali si shwali. Mfano jana, ameamrisha kufanyika maandamano kwa siku tatu bila kupumzika, akilenga bandari kufungwa pamoja na mipaka. Kumeitikiwa kwa muitikio mkubwa katika miji yote mikubwa ya Maputo, Beira, na Nampula pamoja na miji mingine midogo, huku karibu watu 40 wakiwa wameuwawa na polisi.

Inchi inaongozwa na mtu aliyeko mafichoni, huku Rais Nyusi akiwa hana sauti. Ukiona mwenzako ananyolewa.

Soma, Pia: Yanayojiri kwenye Uchaguzi Mkuu wa Msumbiji: FRELIMO (Chama rafiki ya CCM) kushinda Uchaguzi 09 Oktoba?
 
Mbowe angelenda kura za chadema namna hii
 
Saa100 akamsalimie
 
Hata Mackron alikutana na maandamano!
Ni kweli kabisa unachosema, Ila kumbuka kwamba Msumbiji siyo Ufaransa.
Nchini Ufaransa kuna Utawala wa kidemokrasia iliyotamalaki, lakini siyo nchini Msumbiji.

Aidha, utawala au serikali iliyopo Ufaransa imewekwa madarakani na Wananchi, na Serikali ya huko inawajibika kwa Wananchi wa nchi hiyo ya Ufaransa. Lakini nchini Msumbiji Serikali iliyopo huko kamwe haijawahi kuwekwa madarakani na Wananchi wa Msumbiji, na Wala Serikali hiyo haiwajibiki kwa Wananchi.

Kwa kifupi ni kwamba, Serikali ya Msumbiji kamwe haijawahi kupata ridhaa ya kiutawala kutoka kwa Wananchi wa nchi hiyo.
 
Yaani Frelimo ndiyo basi tena,Mungu atuepushe waache kiburi ili kunusuru maisha ya wanaichi,
Viongozi wamejifungia ndani wamebaki kuwatuma polisi kwenda kupiga raia,lakini polisi bado wao kwa wao wanasigana wengine wanasema hawa raia tunaowauwa tunaishi nao na ni ndugu zetu itakuwaje tukiludi majumbani kwetu?
Baadhi ya raia wanawanoti polisi wanaouwa waandamanaji na wanawafwata majumbani kwao kwenda kuwachomea nyumba zao,yaani yanayoendelea huku yanatisha
 
The beginning of the end of FRELIMO.
 
Vyama vya ukombozi vimegeuka vyama vya kiimla..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…