Unaweza kudhani tuko salama mikononi mwa rais Magufuli lakini ni salama kiasi gani hakuna aliye na hakika.
Mafisadi na waliolewa uongozi wanaweza kufanya chochote, hata kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye pia usishangae hii ikafanywa na wabunge toka vyama vyote hasa kwa kuwa rais amekuwa akigusa pia masilahi ya wabunge kuanzia mikopo ya magari ya wabunge hadi juzi bilioni 6 zilivyoondolewa ktk mfuko wa bunge na Magdalena Sakaya akalalamikia kitendo hicho, kuna possibility kwamba linapokuja swala la maslahi ya wabunge uzalendo na vyama huwekwa pembeni.
Rai yangu kwa wabunge wazalendo kutoka vyama vyote utakapofika wakati wa 'masia' kutundikwa msalabani chondechonde nawaomba sana msimame nyuma ya rais wetu mpendwa mkombozi wa wanyonge nnahakika 90%+ ya wananchi watamsupport ili kuhakikisha ukombozi kamili wa nchi hii unapatikana.
Kuna ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya wabunge wetu ni wale wanaojua kuwa tumewapa ubunge kama zawadi na si wao kutuongoza kututoa katika umaskini na shida za sampuli mbalimbali zilizokithiri.
Kama ikitokea bunge likavunjwa nna imani baragumu litakalopigwa na Magufuli kutafuta kuungwa mkono, watakaokuwa nyuma yake ni wabunge ambao wao watakuwa wamejitathmini na kuona kuwa wataendana na kariba ya rais wetu ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wananchi na si kwa masilahi ya chama kwanza.
Naomba kunukuu maneno ya busara kwamba;-
"Don't run after happiness but make other people happy and you will find happiness is running after you" kwamba, tusitafute kujifurahisha wenyewe badala yake tuwafurahishe wengine kisha furaha yenyewe itakuja ikitukimbilia.
Hivi kuna propaganda gani yenye nguvu ya kujenga chama badala ya hii ya kutumikia wananchi kizalendo kama anavyofanya Rais wetu Ndugu John Pombe Joseph Magufuli?