Hata Yanga wanamuhitaji Haji Manara

Efendi

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
314
438
Hata Yanga wanamuhitaji Haji Manara..

Kalamu ya Ally Kamwe

Ni 2016. Kwa haraka haraka sikumbuki siku wala saa, ila ni ndani ya mwaka huo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na kuzungumza na HAJI SUNDAY MANARA.

Ni pale Sinza Kijiweni. Ndani ya jengo kubwa jeupe lenye nuru ya nje, yanapotengenezwa magazeti maarufu Tanzania. DIMBA, BINGWA na MTAZANIA. Naizungumzia Kampuni ya New Habari Corporation.

Kwa dakika 30 nilizomsikiliza Haji Manara kwenye interview (Mahojiano) yake na kundi la waandishi wa habari, niligundua mambo matatu kuhusu yeye.

1: Ni mtu mwenye kinywa kisichotabirika. Anaweza kusema lolote bila kujali chochote. Iwe ametoa hoja ya maana au isiyo na maana, ataihitimisha kwa cheko lake la kibeberu. Ilimradi tu awatoe watu mchezoni.

2: Hakuwa na utulivu wa maneno. Ni kama mtu anayefikiria baada ya kusema. Sekunde anaweza kusema hili. Sekunde chache baadae, neno lilelile akalisema kwa maana nyingine. Inahitaji utulivu sana kumuelewa.

3: Haji anaipenda sana kazi yake. Anaiamini nguvu yake. Anajivunia madhaifu yake. Kwa vyovyote vile tunavyomuona na kumtafsiri, yeye anapenda kuonekana zaidi ya hivyo.

Ukimuona 'Limbukeni', basi yeye huwa 'Limbukeni maradufu'. Huyu ndie Haji Manara.

Mwerevu mmoja aliwahi kusema, Askari jasiri, mwenye nguvu na kila aina ya bastola, si lolote mbele ya muuaji dhaifu anayeipenda kazi yake. Tukifika mwisho wa andiko hili, nitakueleza maana ya msemo huo.

Leo, Januari Mosi, 2019. Miaka miwili na nusu tangu nizungumze nae, kuna kitu kimebadilika kwa Haji Manara.

Tabia zake ni zilezile. Lakini sio yule tena. Kwa sasa ni mtu mwenye ushawishi zaidi kwenye sekta ya michezo Tanzania. Hakuna hata anayemkaribia. Tusiwe wanafki kwenye hili.

Haji amefikaje hapa? Bila shaka nyuma yake amepata watu makini (Managers) waliojua jinsi ya kuutumia 'Ulimbukeni' wake kuitengeneza Brand yake.

Ni watu hao waliomfanya Haji awe kipofu mwenye macho matatu. Si bahati mbaya kumkuta Haji akizungumza kuhusu Soka, Siasa, Muziki hadi udaku wa kina Amber Rutty.

Haji wa sasa sio msemaji wa Simba tu. Bali anatengenezwa kuwa msemaji wa Taifa. Msemaji wa kila kitu. Na inamlipa.

Hivi sasa ni balozi wa kampuni ya Asas na anendelea kukusanya madili mengi nje ya Simba. Huyu ndie Haji tunaemcheka kwa 'Ulimbukeni wake'.

Kimsingi Haji amejua kuitumia vyema nembo ya Simba kujiongeza, lakini nyuma ya pazia Simba wananufaika sana na kinywa cha Haji Manara. Kivipi? Nisikilize kwa makini hapa.

Kwa sasa ni watu wawili tu wakitamka majina yao, taswira ya Simba SC inakujia kichwani. Bilionea Mo Dewji na Haji Manara.

Haji ni Simba. Simba ni Haji Manara. Ni ngumu sana kutenganisha hivi vitu.

Wapi Simba wananufaika na nguvu ya Haji? Kwanza ni kwenye thamani ya nembo yao. Haji anaizungumza Simba kama mtu mwingine anavyoweza kuizungumza Real Madrid au Manchester United.

Haji ameitengeneza Simba kuwa kitu fulani cha thamani, kikubwa cha kuogopwa. Alianza kama utani kusema, Simba ndio klabu yenye mashabiki wengi Tanzania.

Kama utani, uongo ule ukasemwa sana mpaka umeshafanana na ukweli. Hakuna tena msomi anayeweza kusimama na kusema tofauti na hivyo tena. IMESHAAMINIKA SIMBA NDIO KLABU YENYE MASHABIKI WENGI TANZANIA.

Hii sumu imekwenda na kuota mizizi kwenye vifua vya mashabiki. Hivi umeshawahi kumsikia Shabiki wa kawaida Simba akiongea kuhusu timu yake kwenye meza ya magazeti? Utashangaa.

Hata kama hana senti mfukoni lakini utauhisi utajiri na ukubwa wa Simba kwenye kinywa chake.

Ni yuleyule 'Limbukeni' Haji ndio ameifikisha hapo BRAND ya Simba SC. Hakuna mwingine.

Hii ni faida moja ya nje ya uwanja. Twende ndani ya uwanja.

Huku nako Haji ameichukua dhamana ya Simba kwa chochote kitakachotokea, mtu anayetakiwa kuulizwa na kujibu ni yeye. Hakuna tena presha kwa kocha wala wachezaji.

Simba anafungwa na Mashujaa FC na kundi kubwa la watu linawasha data kwa ajili ya kujibizana na Manara na si kuongelea makosa wa Paul Bukaba na Dida.

Kama kuna usajili wa hovyo Simba imefanya basi ni yule Zana Coulibaly. Lakini nani anajali? Kila mtu yuko bize kushambuliana na Haji Manara.

Jaribu kuwaza Haruna Niyonzima ndio angekuwa na takwimu za Ibrahim Ajib? Jaribu kuwaza Mabao ya Makambo yangekuwa kwa Meddie Kagere? Jaribu kuwaza taratibu tu yule Paul Goefrey 'Boxer' angekuwa mchezaji wa Simba? La haula, pengine na gari angeshanunuliwa!!

Ni kinywa cha Haji Manara ndio kinafanya baadhi yetu tumuone Cletous Chama kama Malaika!

Nani anajua kuwa Kichuya ameshuka kiwango? Lakini habari za Tshishimbi zipo kila mahala. Hii ndio faida ya Haji Manara. Kuna utulivu mkubwa sana Simba hivi sasa.

Kwanini naamini Yanga pia wanatakiwa kuwa na mtu kama Manara? Ziko sababu mbili. Ndani na nje ya uwanja.

Nje ya uwanja nembo ya Yanga imenajisikia. Wawekezaji wanaiogopa. Mambo mengi ya hovyo yanatoka nje pasina mipaka.

Leo utaskia stori za kiongozi kupiga hela. Kesho utasikia stori ya mchezaji kudai. Hujakaa sawa, utakumbushwa kuwa kuna bakuli la michango linatembezwa. Hii si taswira nzuri kwa Klabu kubwa kama Yanga.

Katika kipindi hiki cha mpito Yanga inahitaji mwanamume mmoja wa kutuliza mambo kibabe. Yanga inahitaji mtu wa kuja kuisaficha nembo ya klabu na kurejesha thamani yake.

Si kwa bahati mbaya mashabiki hawaendi uwanjani japo timu inapata matokeo na kuongoza Ligi. Watu hawajihisi wa thamani kuvaa jezi ya Yanga.

Huko ni nje ya uwanja. Ndani ya uwanja Yanga inahitaji utulivu mkubwa kuliko kipindi chochote kile.

Kwa kusua sua hivyo hivyo, wanakaribia kuingia raundi ya pili wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi 5. Hii ni advantage kubwa sana kwao.

Nini wafanye? Wanahitaji mtu wa kumpokea kijiti Mwinyi Zahera. Kocha hatakiwi kuzungumza wala kulalamika tena. Focus yake iwe kwenye maandalizi tu.

Haya masuala ya ratiba kubana, mchezaji kugoma, uchaguzi yanatakiwa yawe na Mwanamume wa pembeni wa kupambana nayo.

Yanga inahitahi mtu wa kupelekeshana na TFF kuhusu ratiba. Mtu wa kuzungumza na kuwapa morali wachezaji na mashabiki.

Rafiki yangu Dismas Ten ni mtu sahihi kiutendaji lakini anaangushwa na tamaduni, desturi na ustaarabu wetu wa Kitanzania. Ndio ukweli huo.

Vitu vyote alivyobuni kwa ajili ya Yanga vimeyeyuka kama si kupotea. Jarida hazikuwa na manufaa yoyote kwa Klabu.

Ziko wapi kalenda za Yanga? Ule mfumo wa kuuza jezi mitandanoni umeishia wapi? Website inaenda kwa kusuasusa. Kimsingi Hakuna hata mpango mmoja wa Dismas Ten uliofanikiwa.

Kwanini anafeli? Haukuwa ustaarabu wa timu zetu za Kariakoo. Yanga haiwezi kufanya kazi kama Borrusia Dortmund au Juventus kabla ya kuvuka kwenye desturi yao.

Jaribu kuwaza, Simba wenye Haji Manara wangempata mtendaji kama Dismas Ten, wangeteneza pesa kiasi gani? Tusimdharau Haji moja kwa moja tutakosa nafasi ya kujifunza kitu kutoka kwake.

Haji mmoja ana ushawishi wa kuhamasisha Maelfu ya Wanasimba wakajaa uwanjani, angeshindwa vipi kuuza bidhaa za klabu?

Haji angecharuana na TFF kuhusu ratiba. Angecharuana na mashabiki wanaomponda Kindoki. Angecharuana na kila mtu kwa ajili ya maslahi ya Yanga.

Haya anayoyafanya akiwa Simba sio ya kupuuzwa. Kwani unafikiri yeye hajui kuwa AL AHLY au AS VITA ni imara kuliko Simba? Au yeye hajui maana ya neno 'underdog' kwenye soka?

Anajua sana. Ila asichotaka ni hiyo mentality ienee kwa mashabiki na wachezaji. Wanaweza kukosa pesa ya viingilio na matokeo kama wataukubali huo udhaifu kipindi hiki.

Haji Manara ni muuaji dhaifu anayeipenda kazi yake. Na si ajabu tukiona akishinda kila vita.

Happy New Year Familia yangu ya michezo.

Wenu Ally Kamwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me nimefurahia uchambuzi wako, umekuwa mwandishi mzuri sana. Haji Manara popote anapotajwa naiona simba ile paleee
 
nimependa tu mtiririko wa story yako. uko vizuri kwenye uandishi
 
Ni makala nzuri, lakini imejengwa zaidi kwenye makadirio (assumptions) ambayo sil lazima kila mtu akubaliane nayo (subjective arguments). Kwa mfano, kusema usajili wa beki Coulibaly ni wa ovyo, au kwamba watu wote wanaamini kwamba Simba ndiyo inayoongoza kwa mashabiki, au kwamba wapenzi wa Yanga hawapendi tena kubadili jezi za timu yao, n.k. Ameegemea pia kwenye majaribio ya kifikra (thought experiment) kwamba, mathalan, Boxer angekuwa Simba angekwishanunuliwa gari kwa mdomo wa Manara. Na kwa sababu hoja za aina hiyo ndiyo muhimili wa makala yenyewe, wenye mawazo tofauti na kauli kama hizo wanaweza wasikubaliane na makala yenyewe,
Ila ni makala ya kuvutia, inayoonesha namna Kichwa cha habari kinavyotumika kuvuta hisia za wasomaji lakini bado kikawa kinanedna ana maudhui ya makala yenyewe. Aidha, kuna mtiririko mzuri wa uwasilishaji hoja na lugha isiyoudhi hata kama ujumbe wake haufurahishi. Ni makala stahiki kwa Jukwaa maridhawa kama JF.
 
Mi naamini uwekezaji ulofanywa na MO ndo umeongeza mafanikio kwa haji manara.. Kwamaana hapo kabla pia haji alijitahd sana kuipigania simba yake lakin alionekana tu kituko kwenye ulimwengu wa soka.. Hii ni kwasababu ukweli haujifichi na simba haikuwa bora wakat huo..

Kila mtu anamacho na anaona huwezi kumwambia yanga hii ni bora wakat yeye mwenyew anajionea jinsi inavyopata ushindi kwa tabu.. Hiv vilabu viwili mashabiki huangalia sana hali ya wakat husika kuliko maneno maneno.. Ndo mana kipind cha manji yanga iliingiza watu wengi kuliko simba..

Kwa kumalizia niseme tu yanga haimuhitaj manara inamuhitaj mtu kama MO au uwekezaj mkubwa ili iweze kupata mafanikio coz ata haji manara umaarufu wake unaongezeka kwasabab ya ubovu wa yanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika fikra zangu. Haji ametia ujasiri sana mashabiki wa Simba. This is Simba,juzi Nkana walipokuja alianzisha kauli mbiu ya Kufa na Kupona,ila hamasa ilitia ujasiri uwanja ukatapika
 
Unayo sababu ya kuamini hivyo. Na wengine wanayo sababu ya kuamini kwamba kuna kasoro katika uendeshaji wa Simba (na Timu zetu nyengine) inayomfanya mtu mmoja na mdomo wake usio breki kuwa maarufu kuliko Simba yenyewe, na hivyo kujenga ngome ya kujitengenezea kipato kupitia Klabu yenyewe na bila ya kuyagawana na klabu. Hili halipaswi kutokea popote pale kwenye klabu inayoendeshwa ipasavyo. Nani anaweza kutuambia msemaji wa Man U, au Real Madrid, au timu yoyote yenye mfumo unaoeleweka wa uendeshaji ni nani. Na kama msemaji huyo yupo, tuambiwe ana mikataba gani ya udhamini nje ya klabu hizo. Na tuambiwe nani ni meneja wa msemaji huyo (kumbuka tumeambiwa Manara ana watu wanaomwongoza vizuri). Nani anaweza kutuambia ni kiongozi gani ndani ya timu za aina hiyo ya uendeshaji uliokomaa aliyejijengea umaarufu kwa kuisifia klabu yake (mf. Barcelona) na kwa kuinanga timu ya mtani wake wa jadi (mf. Real Madrid)? Na kama yuko, tuambiwe amejijengea umaaruufu kiasi gani, ana mikataba mingapi ya udhamini nje ya klabu, na mdhamini wake ni nani. Nani anaweza kutambua ni kiongozi gani wa klabu hizo zoefu amebeba jukumu la kuhamasisha washabiki jukwaani kiasi cha kumwaga radhi uwanjani, na hali hiyo imezisaidiaje klabu na yeye mwenyewe. Kwa upande mwengine, tunaona jinsi watu kama Christiano Ronaldo, Messi na kama hao ambao wana umaarufu mkubwa ndani ya timu zao jinsi umaarufu huo unapozaa mapato yanavyogawiwa kwa uwiano mwadilifu baina ya klabu na mhusika. Kwa hivyo kadri tunavyomsifu Manara kwa kuutumia vyema uhamnazo wake ndani ya Simba kupiga madili nje ya Simba, ndivyo tunavyozidi kukubali kwamba kuna uhamnazo zaidi ndani ya Simba (na klabu nyengine zenye wasemaji wa aina hiyo) kuliko alio nao Manara mwenyewe.
 
Haji Manara alikoga chupa za mikojo Kirumba ..walivyoliwa twako na Mbao
 
Yanga inahitaji mwekezaji sio Manara km huyo mtu angekuwa ana mtoto miaka mi3 iliopita alikuwa wapi kufanya yote hayo!
Simba Kuna pesa ndio maana kunavutia hata mashabiki uchwara nao wapo saa hz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Yanga wanamuhitaji Haji Manara..

Kalamu ya Ally Kamwe

Ni 2016. Kwa haraka haraka sikumbuki siku wala saa, ila ni ndani ya mwaka huo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na kuzungumza na HAJI SUNDAY MANARA.

Ni pale Sinza Kijiweni. Ndani ya jengo kubwa jeupe lenye nuru ya nje, yanapotengenezwa magazeti maarufu Tanzania. DIMBA, BINGWA na MTAZANIA. Naizungumzia Kampuni ya New Habari Corporation.

Kwa dakika 30 nilizomsikiliza Haji Manara kwenye interview (Mahojiano) yake na kundi la waandishi wa habari, niligundua mambo matatu kuhusu yeye.

1: Ni mtu mwenye kinywa kisichotabirika. Anaweza kusema lolote bila kujali chochote. Iwe ametoa hoja ya maana au isiyo na maana, ataihitimisha kwa cheko lake la kibeberu. Ilimradi tu awatoe watu mchezoni.

2: Hakuwa na utulivu wa maneno. Ni kama mtu anayefikiria baada ya kusema. Sekunde anaweza kusema hili. Sekunde chache baadae, neno lilelile akalisema kwa maana nyingine. Inahitaji utulivu sana kumuelewa.

3: Haji anaipenda sana kazi yake. Anaiamini nguvu yake. Anajivunia madhaifu yake. Kwa vyovyote vile tunavyomuona na kumtafsiri, yeye anapenda kuonekana zaidi ya hivyo.

Ukimuona 'Limbukeni', basi yeye huwa 'Limbukeni maradufu'. Huyu ndie Haji Manara.

Mwerevu mmoja aliwahi kusema, Askari jasiri, mwenye nguvu na kila aina ya bastola, si lolote mbele ya muuaji dhaifu anayeipenda kazi yake. Tukifika mwisho wa andiko hili, nitakueleza maana ya msemo huo.

Leo, Januari Mosi, 2019. Miaka miwili na nusu tangu nizungumze nae, kuna kitu kimebadilika kwa Haji Manara.

Tabia zake ni zilezile. Lakini sio yule tena. Kwa sasa ni mtu mwenye ushawishi zaidi kwenye sekta ya michezo Tanzania. Hakuna hata anayemkaribia. Tusiwe wanafki kwenye hili.

Haji amefikaje hapa? Bila shaka nyuma yake amepata watu makini (Managers) waliojua jinsi ya kuutumia 'Ulimbukeni' wake kuitengeneza Brand yake.

Ni watu hao waliomfanya Haji awe kipofu mwenye macho matatu. Si bahati mbaya kumkuta Haji akizungumza kuhusu Soka, Siasa, Muziki hadi udaku wa kina Amber Rutty.

Haji wa sasa sio msemaji wa Simba tu. Bali anatengenezwa kuwa msemaji wa Taifa. Msemaji wa kila kitu. Na inamlipa.

Hivi sasa ni balozi wa kampuni ya Asas na anendelea kukusanya madili mengi nje ya Simba. Huyu ndie Haji tunaemcheka kwa 'Ulimbukeni wake'.

Kimsingi Haji amejua kuitumia vyema nembo ya Simba kujiongeza, lakini nyuma ya pazia Simba wananufaika sana na kinywa cha Haji Manara. Kivipi? Nisikilize kwa makini hapa.

Kwa sasa ni watu wawili tu wakitamka majina yao, taswira ya Simba SC inakujia kichwani. Bilionea Mo Dewji na Haji Manara.

Haji ni Simba. Simba ni Haji Manara. Ni ngumu sana kutenganisha hivi vitu.

Wapi Simba wananufaika na nguvu ya Haji? Kwanza ni kwenye thamani ya nembo yao. Haji anaizungumza Simba kama mtu mwingine anavyoweza kuizungumza Real Madrid au Manchester United.

Haji ameitengeneza Simba kuwa kitu fulani cha thamani, kikubwa cha kuogopwa. Alianza kama utani kusema, Simba ndio klabu yenye mashabiki wengi Tanzania.

Kama utani, uongo ule ukasemwa sana mpaka umeshafanana na ukweli. Hakuna tena msomi anayeweza kusimama na kusema tofauti na hivyo tena. IMESHAAMINIKA SIMBA NDIO KLABU YENYE MASHABIKI WENGI TANZANIA.

Hii sumu imekwenda na kuota mizizi kwenye vifua vya mashabiki. Hivi umeshawahi kumsikia Shabiki wa kawaida Simba akiongea kuhusu timu yake kwenye meza ya magazeti? Utashangaa.

Hata kama hana senti mfukoni lakini utauhisi utajiri na ukubwa wa Simba kwenye kinywa chake.

Ni yuleyule 'Limbukeni' Haji ndio ameifikisha hapo BRAND ya Simba SC. Hakuna mwingine.

Hii ni faida moja ya nje ya uwanja. Twende ndani ya uwanja.

Huku nako Haji ameichukua dhamana ya Simba kwa chochote kitakachotokea, mtu anayetakiwa kuulizwa na kujibu ni yeye. Hakuna tena presha kwa kocha wala wachezaji.

Simba anafungwa na Mashujaa FC na kundi kubwa la watu linawasha data kwa ajili ya kujibizana na Manara na si kuongelea makosa wa Paul Bukaba na Dida.

Kama kuna usajili wa hovyo Simba imefanya basi ni yule Zana Coulibaly. Lakini nani anajali? Kila mtu yuko bize kushambuliana na Haji Manara.

Jaribu kuwaza Haruna Niyonzima ndio angekuwa na takwimu za Ibrahim Ajib? Jaribu kuwaza Mabao ya Makambo yangekuwa kwa Meddie Kagere? Jaribu kuwaza taratibu tu yule Paul Goefrey 'Boxer' angekuwa mchezaji wa Simba? La haula, pengine na gari angeshanunuliwa!!

Ni kinywa cha Haji Manara ndio kinafanya baadhi yetu tumuone Cletous Chama kama Malaika!

Nani anajua kuwa Kichuya ameshuka kiwango? Lakini habari za Tshishimbi zipo kila mahala. Hii ndio faida ya Haji Manara. Kuna utulivu mkubwa sana Simba hivi sasa.

Kwanini naamini Yanga pia wanatakiwa kuwa na mtu kama Manara? Ziko sababu mbili. Ndani na nje ya uwanja.

Nje ya uwanja nembo ya Yanga imenajisikia. Wawekezaji wanaiogopa. Mambo mengi ya hovyo yanatoka nje pasina mipaka.

Leo utaskia stori za kiongozi kupiga hela. Kesho utasikia stori ya mchezaji kudai. Hujakaa sawa, utakumbushwa kuwa kuna bakuli la michango linatembezwa. Hii si taswira nzuri kwa Klabu kubwa kama Yanga.

Katika kipindi hiki cha mpito Yanga inahitaji mwanamume mmoja wa kutuliza mambo kibabe. Yanga inahitaji mtu wa kuja kuisaficha nembo ya klabu na kurejesha thamani yake.

Si kwa bahati mbaya mashabiki hawaendi uwanjani japo timu inapata matokeo na kuongoza Ligi. Watu hawajihisi wa thamani kuvaa jezi ya Yanga.

Huko ni nje ya uwanja. Ndani ya uwanja Yanga inahitaji utulivu mkubwa kuliko kipindi chochote kile.

Kwa kusua sua hivyo hivyo, wanakaribia kuingia raundi ya pili wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi 5. Hii ni advantage kubwa sana kwao.

Nini wafanye? Wanahitaji mtu wa kumpokea kijiti Mwinyi Zahera. Kocha hatakiwi kuzungumza wala kulalamika tena. Focus yake iwe kwenye maandalizi tu.

Haya masuala ya ratiba kubana, mchezaji kugoma, uchaguzi yanatakiwa yawe na Mwanamume wa pembeni wa kupambana nayo.

Yanga inahitahi mtu wa kupelekeshana na TFF kuhusu ratiba. Mtu wa kuzungumza na kuwapa morali wachezaji na mashabiki.

Rafiki yangu Dismas Ten ni mtu sahihi kiutendaji lakini anaangushwa na tamaduni, desturi na ustaarabu wetu wa Kitanzania. Ndio ukweli huo.

Vitu vyote alivyobuni kwa ajili ya Yanga vimeyeyuka kama si kupotea. Jarida hazikuwa na manufaa yoyote kwa Klabu.

Ziko wapi kalenda za Yanga? Ule mfumo wa kuuza jezi mitandanoni umeishia wapi? Website inaenda kwa kusuasusa. Kimsingi Hakuna hata mpango mmoja wa Dismas Ten uliofanikiwa.

Kwanini anafeli? Haukuwa ustaarabu wa timu zetu za Kariakoo. Yanga haiwezi kufanya kazi kama Borrusia Dortmund au Juventus kabla ya kuvuka kwenye desturi yao.

Jaribu kuwaza, Simba wenye Haji Manara wangempata mtendaji kama Dismas Ten, wangeteneza pesa kiasi gani? Tusimdharau Haji moja kwa moja tutakosa nafasi ya kujifunza kitu kutoka kwake.

Haji mmoja ana ushawishi wa kuhamasisha Maelfu ya Wanasimba wakajaa uwanjani, angeshindwa vipi kuuza bidhaa za klabu?

Haji angecharuana na TFF kuhusu ratiba. Angecharuana na mashabiki wanaomponda Kindoki. Angecharuana na kila mtu kwa ajili ya maslahi ya Yanga.

Haya anayoyafanya akiwa Simba sio ya kupuuzwa. Kwani unafikiri yeye hajui kuwa AL AHLY au AS VITA ni imara kuliko Simba? Au yeye hajui maana ya neno 'underdog' kwenye soka?

Anajua sana. Ila asichotaka ni hiyo mentality ienee kwa mashabiki na wachezaji. Wanaweza kukosa pesa ya viingilio na matokeo kama wataukubali huo udhaifu kipindi hiki.

Haji Manara ni muuaji dhaifu anayeipenda kazi yake. Na si ajabu tukiona akishinda kila vita.

Happy New Year Familia yangu ya michezo.

Wenu Ally Kamwe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni miongoni mwa makala za ovyo kabisa ambazo nimewahi kuziona katika maisha yangu...yaani mtu mropokqaji anasifiwa ??!! eti mtu anayewadhalilisha wengine anasifiwa??!! Mtu kama huyu nchi nyingine angekuwa tayari ameshafungiwa...Kwamba huyo jamaa bado yupo kwenye nafasi hiyo ni kutokana na mfumo mbaya siyo wa soka tu bali hata jamii nzima kwa ujumla wake...jamii yetu inayopenda mipasho, gossips, majungu na uropokaji..mfumo wetu ndio unaotaka watu wa aina hii...Hata yanga miaka siyo mingi walikuwa na mtu wa aina hiyo...hivi unadhani neno la 'wa kimataifa' lilianzia wapi?? 'wa matopeni' lilikujaje?? Watu wakawa wanapenda mipasho ya aina hii...badala ya kuchambua soka, jamii yetu inapenda habari za 'kukwea pipa'...Yaani watu wazima na akili zetu tunakaa kujadili vijiweni eti sasa 'timu yetu inapanda ndege'...it is no wonder soka ya Tanzania haitaendelea kamwe kwa staili hii...
 
Back
Top Bottom