GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,806
- 9,637
Ni kisa cha kushangaza sana. Nimeikuta mtandao wa Quora.
Baada ya mazishi ya mwanaume mmoja, mbwa wake alitoweka ghafla na kwenda kusikojulikana. Siku mbili baadaye alikutwa akiwa amelala kwenye shimo alilolichumba juu ya kaburi la marehemu. Kijana wa marehemu alimchukua na kumrejesha nyumbani.
Siku mbili baadaye alitoroka tena na kurudi kwenye kaburi la marehemu, ambaye ndiye mtu aliyekuwa akimmiliki huyo mbwa kabla ya kukutwa na mauti.
Baada ya kijana wa marehemu kusumbuka naye kwa siku kadhaa kumrudisha nyumbani bila mafanikio, kwani kila alupomrudisha alitoroka tena na kurudi kaburini, aliamua kumwacha huko makaburini. Akawa anampelekea kila siku chakula na maji. Hata hivyo aligoma kula.
Kwa kipindi chote alichokaa hapo kaburini, hakuwa akimruhusu mtu yeyote kulisogelea hilo kaburi isipokuwa kijana wa marehemu. Alililinda kaburi kwa ukali na umakini wa hali ya juu. Sijui alikuwa akifikiri marehemu atafufuka!
Wiki moja baadaye baada ya kuachwa kukaa makaburini full time, huyo mbwa naye alikufa akiwa juu ya kaburi la "bosi" wake.
Mbwa alimpenda sana aliyempenda. Alimwombolezea "rafiki" yake hadi naye akafa akiwa katika majonzi.
Hata wanyama wanaweza kuonesha hisia za upendo na za huzuni.
Tujifunze kuwathamini.