RIGHT MARKER
Member
- Apr 30, 2018
- 88
- 336
Mhadhara 31:
Leo naomba niwajuze abiria wa daladala jambo ambalo makondakta wamesomea CUBA, na jinsi ambavyo wanatumia vizuri D2 za shuleni.
1. Matumizi ya D2:
Kumbukumbu walizonazo makondakta (tingo) za kuwakumbuka abiria wote ambao tayari wamewatoza nauli, na abiria ambao bado hawajawatoza nauli. Kwenye hili naamini makondakta wote wana D2 za Historia na Hisabati. Kwasababu si rahisi kondakta kumsahau kumdai abiria nauli hata kama abiria ataingia kupitia dirishani.
2. Walichosomea CUBA:
Kuna hiki kitu ambacho makondakta wamekisomea CUBA na huenda baadhi ya abiria hawajakigundua hasa kwa wale abiria wa mabus madogo ya mikoani. Kondakta (Tingo) anapochukua nauli ya abiria ambayo inahitaji kurudishwa chenji huwa anajichelewesha kurudisha chenji.
Kwa mfano nauli ya safari ni Tsh 1,000, wewe umempa Tsh 5,000 au 10,000; hata kama chenji anazo mkononi kamwe hawezi kukurudishia papo hapo mpaka wewe mwenyewe umkumbushe kondakta, hii ipo sana kwa makondakta wa mikoani tofauti na hapa DSM.
Hapa niwajuze abiria kuwa si kwamba kondakta amesahau kukurudishia chenji yako, bali ile ni mbinu waliosomea makondakta huko CUBA. Unaweza kudhani amesahau kumbe yeye ndo anataka wewe usahau ili iwe faida kwake.
Right Marker
Dar es salaam