Hata kwenye siasa ili upate kibali na amani ni muhimu kusamehe soma kitabu chako cha Dini

howardlite

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
235
372
Zipo kanuni katika maisha ambazo hatuwezi kuzivunja iwe kwa bahati mbaya au makusudi tukabaki bila kuathiriwa kama adhabu ya kuzivunja au kuzipuuza.

Siasa ni jumla ya vitu vingi katika taifa kwa sehemu kubwa vinaamua maisha ya watu ya jana,leo na kesho yao.

Wengi wa Watanzania sio wana siasa,lakini haibadilishi kuwa siasa ndio zinaendesha nchi yetu mpaka tumefika hapa ni zao la siasa pamoja na mambo mengine ambayo yanatajwa kwenye misingi ya ujenzi wa taifa.

Kwa vipindi tofauti vya uendeshaji wa nchi yetu chini ya serekali za awamu zote kupitia siasa yapo maeneo ambayo sehemu ya Watanzania walikufa, walijeruhiwa,waliumizwa na kupitia hali za kuvunja moyo katika mazingira mbalimbali ya harakati za siasa za nchi yetu.

Wengine bado makovu na alama za kihisia,kimwili na kisaikolojia zimeendelea kuacha chuki kubwa kwa wanaoaminiwa kwa namna yoyote ile walihusika na hali hiyo hata kama yaweza kuwa ni mtazamo usio sahihi sana.

Je tuendelee kuwa na uchungu siku zote kwa tuliyotendewa?Ni kweli ni ngumu sana kila tukikumbuka,ni sawa kwakuwa ni wanadamu,lakini kuna mahali Mwenyezi Mungu anatutaka tusamehe,kile anachokisema tukifanye ambacho kwetu ni kigumu yeye ana nguvu ya kutuwezesha kukifanya(kusamehe).

Dini zote zina neno samehe,kusamehe hakuondoi maana tumepitia nini lakini ule uchungu ndio kosa.
Kisasi sio juu yetu ni Mwenyezi Mungu pekee ndio hulipa kisasi.

Kwenye Bible inasema hata ukiwa na sadaka ukikumbuka una neno na ndugu yako iache sadaka mikononi mwa kiongozi wako uende ukatengeneze na ndugu yako ndio urudi uitoe.

Kwenye msahafu ni dhambi moja tu haisamehewi,shiriki lakini hata mtu akiacha bado Mwenyezi Mungu anamsamehe.

Hasira na uchungu kwa watu si kuwa ni dhambi ya kutuzuia tusione mbingu za Mwenyezi Mungu pia huweza kuleta magonjwa kama ya moyo,kiharusi,magonjwa ya akili na ya kisaikolojia.

Jaribu kufikiri kuna faida ya kuendelea kumbeba au kuwabeba hao watu kweye moyo wako. Tafuta kuwa na amani na nafsi yako na watu,hebu tutangaze kuwasamehe kikweli kweli waliotusababishia maumivu na mateso kupitia siasa za nchi yetu iwe kwenye serekali,vyama vyetu,vyombo vya usalama au mazingira yoyote ya siasa na Mungu atatupa amani na kuwa watu wasio wa kawaida kuifaa nchi yetu,atatupa akili njema na maarifa ya kuofanya nchi yetu kuwa nchi bora.

Narudia tena ni ngumu kibinadamu kusamehe lakini kuna nguvu ya kutusaidia kwa faida yetu,familia zetu, vizazi vyetu,taifa letu na kesho yetu peponi. Tukisameheana hatutaendeleza chuki,visasi,matusi,kudhihakiana na vita visivyo na faida.

Sisi sote ni ndugu tunaunganishwa na utaifa wetu na ni waja wa Mwenyezi Mungu,tusameheana maisha ni zaidi ya haya tunayoyaona na kuyapigania.
 
..Tanzania inahitaji Tume ya Ukweli Haki na Maridhiano.
Ni kweli mkuu tukijua kila tunachokipanda tutavuna,tukitendea wengine isivyo haki na sisi tusivyopenda kutendewa maumivu yao ni kisasi kwetu namna nzuri ni kujisahihisha ili sote tuwe salama na amani na tuishi kwa upendo.
 
..waliotenda ubaya wanateseka kwa hatia iliyoko mioyoni mwao na kuficha siri.

Nashauri wote waliotenda ubaya wakiri na kuomba radhi ili kuutua mzigo wa hatia unaowaandama siku zote.

..hata kama hawajulikani na umma lakini ktk nafsi zao wanajua maovu waliyotenda.
 
Back
Top Bottom