Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,201
- 5,584
Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga amesema kabla ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Milton Lupa kimetokea akiwa njiani kuripoti katika wadhifa mpya.
Hasunga amesema alizungumza naye siku tatu kabla kuhusu uhamisho wake kutoka katika kituo chake Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) jijini Dodoma.
Amesema kabla ya kuanza safari walijadili kuhusu masuala ya kampuni yao, ndipo alipompa taarifa ya uhamisho wa kituo cha kazi kwenda Veta.
Hasunga ameyasema hayo leo Juni 7, 2024 wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Moravian, Ushirika wa Mabibo Dar es Salaam, kuwa alitakiwa kuripoti Jumatatu Juni 3, 2024.
"Siku iliyofuata saa 10 jioni nilipokea simu ya kifo cha Lupa na mimi nilimpigia simu mkurugenzi wa Veta kama ana taarifa yoyote ya ajali, alinijibu yuko safarini anatokea Dar es Salaam kwenda Dodoma na hana taarifa yoyote hivyo alisema atapita eneo la tukio kwa kuwa hakuwa mbali na eneo hilo," amesema.
Pichani, Japhet Hasunga katikati wakati huo akiwa waziri wa kilimo akiwa na Milton Lupa(kulia) wakati akiwa mtendaji mkuu NFRA. Walikuwa kwenye tukio la kuzindua bodi mpya ya kushauri NFRA kujiendesha kwa faida.(Picha kutoka Maktaba)
Pia, soma=> Inakuwaje Marehemu Milton Lupa anateuliwa mkeka mpya wa Rais?