Pre GE2025 Hashim Rungwe: Kama wanajeshi wanapata chakula, wanafunzi wapewe pia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,877
5,051
Hashim Rungwe Spunda, Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Taifa kuhusu Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kupata chakula na huku akiona hakuna umuhimu wakuwa na Jeshi hilo na akipendekeza pia Wanafunzi wapewe chakula.

 
Fala kweli eti anamsifia Kikwete peke yake, ana Uzuzu haoni kazi nzuri ya Rais SSH awamu hii kila pahala panajengwa
 
Kwa nini JKT wanalishwa na serikali??
Ni Watu wazima hao ambao wapo kambini kwa shughuli maalum, ingekuwa sio kulishwa ilibidi wapewe ujira wakajinunulie chakula
Hao na wanaume na wanawake ambao hawapo chini ya himaya ya wazazi wao......na as long as agenda yao ni jeshi basi serikali inawajibika kwa hilo
 
yupo sahihi, Nchi nyingi za dunia ya pili na ya tatu watoto huwa wanapata posho zao. tunashindwa ku focus na mambo ya msingi tup bzy na mambo yasio ya msingi. Tuna tatizo kubwa la vipaumbele kama taifa.
 
Nini kiliondoa chakula secondary? Enzi za mwinyi/nyerere shule ulikuwa unaenda na bakuli/sahani/kijiko/kikombe mnakula free ,alivyoingia Mkapa akaondoa ...sijui sababu ilikuwa nini.

Enzi za Nyerere/Mwinyi daftari likiisha unapelekwa kwa mwalimu anakupa jipya.
 
Uzae wewe afu serikali ikulishie mwanao?
Serikali zote zenye akili duniani zinawapa chakula bora kabisa wanafunzi mashuleni kupitia kodi ya raia.

Mtoto akidumaa mwili au akili kwa sababu ya lishe mbovu ni hasara kwa taifa zima.
 
Back
Top Bottom