Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,966
- 5,348
Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, ametangaza kuwa atamalizia ujenzi wa msikiti ambao Diamond Platnumz aliuanzisha kijijini kwao Mtwara mwaka 2018. Kupitia Insta Story yake, Harmonize amesema kuwa msikiti huo ulianzishwa baada ya wao wawili kujadili umuhimu wa kusaidia jamii na kuwekeza mbele za Mungu.
Kwa mujibu wa Harmonize, Diamond alimpatia pesa za kuanzisha msikiti huo, lakini baadaye mradi huo ulisimama kutokana na changamoto mbalimbali. Hata hivyo, Harmonize amesema kuwa wiki iliyopita aliamua kuchukua hatua na tayari ametoa bajeti yote ili msikiti huo ukamilike kabla ya Sikukuu ya Eid.
Aidha, ameeleza kuwa msikiti huo utaitwa Masjid Naseeb kama njia ya kumshukuru Diamond kwa mchango wake wa awali. "Mungu akuzidishie ndugu yangu, hujapoteza," ameandika Harmonize, akiwatakia waumini wote Ramadhani njema.