Harmonize atumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kuomba msamaha kwa Diamond kwa bifu lao lililotokea, 'Am Sorry'

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,946
5,296
Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, amemuomba msamaha Diamond Platnumz kwa tofauti zilizowahi kutokea kati yao. Kupitia Insta Story yake, Harmonize ameandika kuwa anatumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kuomba msamaha kwa yeyote aliyemkosea, akisisitiza kuwa hana tena nafasi ya kutoelewana na mtu yeyote.

1740904477653.png
"Naungana na waislam wenzangu kumuomba mungu msamaha wa makosa yetu tuliyoyafanya kwa kukusudia na kutokusudia bila shaka mungu mwingi wa kusamehe atatusamehe inshallah. kipekee kabisa nimuombe msamaha yeyote niliye mkosea kwani mimi bado nina sifa za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kukosea!!!"

"Kutoka ndani ya moyo wangu kwa dhati kabisa!! nimemsamehe yeyote tuliyekwazana kwa lolote!! kupitia mwezi huu mtukufu, nitahakikisha kila changamoto na tofauti zozote nazitatua!! namuomba mungu kupitia neema ya mwezi mtukufu wa ramadhani ulete mapatano, maridhiano na kazi ziendelee. kila anaye soma maandiko haya anamchango wa aina yake katika maisha yangu!!!! "

Tarehe 15/ mwezi huu wa tatu inshallah natimiza miaka 31, alhamdulillah namuomba mungu uhai, afya pamoja na riziki ninayostahili. kipekee kabisa sitaki kuhusishwa au kutajwa katika tofauti zozote zile kwani hazimpendezi mungu, binafsi nimezichoka."

"Safari yangu ya zanzibar imenivutia, bila shaka imekuwa kama ukumbusho kwangu kwamba maisha ya upendo ni bora zaidi kwa namna yoyote ile. sikutakiwa kurushiana maneno na my brother naseeb, so sorry my brother, i apologize, nilichelewa kutambua hakuna mkamilifu. tuliyofanya pamoja ni mazuri na ni mengi kuliko shetani aliyekati yetu. sioni haja na faida yake!!!!"

"Mwezi mtukufu wa ramadhani huleta amani na upendo kwa watu wote"

Screenshot 2025-03-02 112526.png
 
Huyu kaona maisha ya diamond. Fun and entertaining ndio maana kaona arudi kundini, anajua atacheza na upepo , kama jux na ommydimpoz. Ameamini starehe atazifanya sana, nje ataruka sana akiwa na kina diamond. Hata mikopo ya milioni 200 hana haja nayo. Ni hela yakutafuta tu. Huyu jembe ni jembe anamtumia tu. Arudi kambini.
 
Kama yametoka moyoni, basi Harmonize ni mtu muungwana mno.

Hakuna ujasiri mkubwa kama kukiri makosa na kuomba msamaha.

Ni binadamu wachache sana wenye uwezo wa kufanya hivi.
Simwamini huyu kijana, akitaka kutoa wimbo ataanza tena drama zake.
Ikiwa amekusudia kubadilika...ninamuombea mema
 
Wasanii umri wao unarudi kinyume nyume. Mimi nipo darasa la kwanza namsikia nature anaimba, sijui hata hawanawake ni nini nasikia skendo za nature na sinta, Nakuwa mkubwa Nature yupo, juzi naona kwenye interview nature anataja miaka yake, eti tunalingana miaka?
 
Kama yametoka moyoni, basi Harmonize ni mtu muungwana mno.

Hakuna ujasiri mkubwa kama kukiri makosa na kuomba msamaha.

Ni binadamu wachache sana wenye uwezo wa kufanya hivi.
Yani sawa na mtu kukuambia ugua pole kwenye social networks ,sijui kwako utauchukuliaje. Maana naona kama kejeli, anaweza kuomba Msamaha bila kuenda kwenye mitandao ya jamii, zaidi ya hapo ni kutafuta kiki,halafu sio mara kwanza kuandika alicho kiandika.

Ommy na Mondi walikuwa na beef,sijui nani alimkosea mwenzake,ila Ommy Dimpoz na Mondi now wapo poa sijaona Ommy au Mondi wakiombana kusameheana kwenye social networks. Bali tuliwaona wanahang pamoja kwenye event nyingi.
 
Wasanii umri wao unarudi kinyume nyume. Mimi nipo darasa la kwanza namsikia nature anaimba, sijui hata hawanawake ni nini nasikia skendo za nature na sinta, Nakuwa mkubwa Nature yupo, juzi naona kwenye interview nature anataja miaka yake, eti tunalingana miaka?
Sio haba harmonize nimempita na miaka minne 😁
 
Back
Top Bottom