Noel france
JF-Expert Member
- Oct 8, 2012
- 1,101
- 907
Kupitia maandishi ya mwana CCM bwana Hamis kigwangalla, napata mashaka makubwa sana. Uwenda wewe ndiye mtu ambaye unawauza viongozi wenzio kwa wenye mamlaka... !
Tumeanza kuwa ma-bro sasa, Vijana Chipukizi na watoto wanatutazama kama viigizo, wanajifunza kwetu, tuwe makini sana.
Kaka yangu Mhe. Lissu anasema kwenye mahojiano yake na BBC kuwa “Anataka kumuokoa Mhe. Mbowe asiwe kama Mugabe…anataka kulinda legacy yake…”
Vijana mjifunze hivi: Ukiwa kwenye siasa usiongee saaana, kuna chance utakosea ama utajichanganya!
Mfano: Mhe. Lissu amekuwa akimkashifu mwenzake kuwa amelamba asali, viongozi wengine wamelamba asali, na kuuaminisha umma wote na wana CHADEMA kuwa aliyebaki safi ni yeye tu! Na hata kwenye mahojiano hayo hayo kuna sehemu amesema “Mwenyekiti aliyeingia jela, siye aliyetoka jela miezi minane baadaye…amebadilika sana!” “Mwenyekiti alipotoka jela alipitilizia Ikulu…na kuna mambo ya Ikulu hajawahi kuwaambia, kwamba siyo kila atakachoongea na Rais ni lazima wajue.”
Kauli zote hizi zinajenga mazingira kwamba Mhe. Mbowe has become too soft, kuna kitu kapewa “amelainika”, na kwamba kukabiliana na CCM panahitajika mabadiliko, na yeye ndiyo mabadiliko yenyewe ya uongozi sasa!
Kama Mhe. Mbowe amelambishwa asali na ndiyo maana amebadilika anaimba ‘maridhiano na mapendano’, Mhe. Lissu anataka kulinda ‘legacy’ ipi sasa ya Mhe. Mbowe?
Kama yeye Mhe. Lissu ndiyo mabadiliko yenyewe, aliposhinda Urais wa TLS alibadilisha kitu gani cha ajabu?
Yeye amekaa miaka 21 kwenye mapambano ya upinzania, uenyekiti ndiyo utaleta tofauti, ambayo ameshindwa kuleta katika miaka yote hii? Kwani kuleta mabadiliko ni mpaka awe Mwenyekiti? Ama kiti kina asali?
I feel for Mhe. Mbowe maskini. Mhe. Mbowe alivyokipigania chama, kwa nguvu za ujana wake, kwa pesa za familia yake, kwa ku-risk kupoteza marafiki na biashara zake, kwa kuswekwa jela na kupigwa vita; alivyowapigania makamanda wake, leo anakuja kuanikwa na kusemwa namna hii kama mhuni mmoja tu?
Tena na mtu aliyemchukua kwa ndege kumkimbiza Agha Khan Nairobi ili kuokoa maisha yake? Akamlinda asimalizwe na wabaya wake?!
Akahamasisha watanzania wamchangie pesa za matibabu na zilizopungua akalipa mwenyewe, leo haya ndiyo malipo yake? I feel for the bro aisee.
Ama kweli ukimfadhili mbuzi utakunywa supu walau…
Mwandishi bwana Hamis kigwangalla