Hamna nchi ngumu kubuni, kuanza na kuendeleza biashara kama Tanzania kwa sasa.

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
9,572
33,428
Kwa uzoefu wangu wa kufanya biashara hapa nchini ni megundua hamna nchi ngumu kulea biashara watoto na wajuku wako waikute, watu wanapoteza mitaji kimasihara, mtu anafungua duka la vipodozi na mtaji wa 150m au vipuri vya gari ndani ya miazi sita tu kufanya stock taking unakuta pesa imekata kutoka 150m kuna 90m tu, unajiuliza kuna mchawi au naibiwa, wakati mtaji huo ukiupeleka Zambia Rwanda Malawi au Namimbia utaheshimika sanaa na utapata faida kubwa kuliko hapa bongo waanya biashara wa Tanzania wa lioko malawi na zambia wana tucheka sisi tulitanguliza uzalendo wakati TRA haina uzalendo.....

Huenda sehemu ya visababisho ni vifuatavyo:

1. Unprecedented govt taxes za serekali ambazo zina buniwa kila ukicha bila kuzingatia hali ya biashara nchini, direct na indirect taxes

2. Kushuka kwa thamani ya Tz shilling kila siku pesa inashuku ila raia wengi hawajagundua sh 10,000 miaka mitatu nyuma sio 10,000 ya leo haina parchasing power tena, huwezi kuacha nyumbani kamatumizi ya siku tena

3. Sera za kisiasa zinazo badilika kila ukicha ni tatixo kubwa marufuku zimekua marufuku kila siku, unaweza ukapoteza mtaji hivi hivi.

4.Riba za benki kubwa ni firisi benki za Tanzania hazisaidii au kujenga mfanya biashara ila zinamfrisi tu na kuchukua dhamana zake.

5. Hulka na mitizamo hasi dhidhi ya wafanyabiashara walio fanikiwa au wenye mtaji mkubwa kdgo wengi wanakua judged na jamii kama wezi, tapeli watoa rushwa hawana public sympathy.

Kama wataka kuanzisha biashara ya mda mrefu Tanzania jifikilie kwanza sana, utakuja kupoteza mtaji bure na utaishia kuokoka na kule wachungaji watakupiga hiyo salio.
 
Mkuu haya yote walaumu CCM. Miaka 60+ ya uhuru lakini utafikiri ni Sudan Kusini iliyopata uhuru miaka 13 iliyopita.

Tanzania chini ya ccm kila kitu kiko hovyo hovyo, sera zisizotekelezeka za kiuchumi, mipango mibaya ya kiuchumi, umasikini, rushwa, ufisadi, ujinga, mipango miji ya hovyo, miji haijapangiliwa, mifumo isiyoeleweka.

Chini ya ccm tusitegemee chochote cha maana kitafanyika.
 
Nchi hoyote watu wanao shikiria uchumi ni wafanya biashara wa kati, sio wana siasa au watumishi ila kwetu hapa mfanya biashara anachukuliwa kua adui wa TRA wanatembea na seal kufunga maduka ya watu kwa furaha, hawati kuelimisha mtu kuhusu hizo kodi mpya ni kumfungia tu, hi nchi ni chagamoto kweli kweli.
 
And nothing will change kama sisi hatutoreact na kuwa kama wakenya hivi karibuni never
 
Hiki kitu wabongo wengi huwa wanachanganya sana, wanaotembea na makufuli na kufunga maduka ni watu wa service levy au halmashauri.

TRA huwa wanapewa lawama sana katika hili na wakati sio wao wanaofanya hivo.
 
Shida myingine kubwa ni CCM kuomba michango ya kampeni na mikutano kila mara. Na wakiwanyima duka halina maisha. Watakuletea polisi, TRA, OSHA ........... Ilimradi tu ufirisike.
 
Njia pekee wanayo tumia hao mnao waita wafanya biashara wa kubwa au wawekezaji ni kujipendekeza kwa chama cha kijani lakini mioyoni mwao moto unawaka …… ukiwa mtu serious bongo kutoboa siyi rahisi ndomana wwngi walio fanikiwa wanafanya magendo
 
Tatizo kubwa linaanzia bungeni wabunge wengi ni watu wanaotoka sekta ya ajira iwe binafsi au serikali na taasisi zake

Hawajui kabisa jinsi private sector inavyotakiwa kuwa wamejaa bungeni ma ex employees tu hadi mawaziri wamejaa ex employees
Bunge likibadilika composition tutaona mabadiliko
 
Swali fikirishi je tuna mfumo wa kiuchumi wa kitaifa ambao akija kiongozi yoyote hawezi kuuchezea?
 
ila kuna wageni wanakuja wanapiga pesa wanaondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…