Halotel huduma kwa wateja wana huduma mbovu mno

The Eric

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
6,303
10,675
Halo,

Na niseme kwamba wahudumu wa mtandao wa simu halotel kitengo cha kupokea simu 100 huduma kwa wateja huwa wana huduma zisizo ridhisha na mbovu kuwahi kutokea.

Sijui wamewaokota wapi hawa wahudumu wao wabovu namna hii,

Kwanza wanatujibu vibaya wateja na wanafoka na mteja hata awe mstaarabu.

Vile vile unapiga simu inaita muda mrefu haipokelewi inakata yenyewe, useless kabisa, system mbovu.

Lingine wanaunganisha wateja na huduma zinazo wakata pesa ambazo mteja hakujiunga nazo kuna huduma yao ya kijinga kabisa inaitwa haloquiz.

Hii nchi ishaanza kuwa ngumu sasa. Kwani nini hawa halotel wasichukuliwe hatua kwa uwizi na kutokuwa waadilifu watakuja kufanya mambo ya cyber crime.

nitaweka mawasiliano yangu
nihojiwe kwa haya kama ipo haja.

Maendeleo hayana CCM wala CHADEMA😅
 
Huu uzi nilishauleta mim Jana malalamiko Kama hayo hiyo haloquiz ni utapeli mtupu huduma ata ukijitoa bado pesa inaendea kukatwa Kila siku Tsh 100
 
Huu uzi nilishauleta mim Jana malalamiko Kama hayo hiyo haloquiz ni utapeli mtupu huduma ata ukijitoa bado pesa inaendea kukatwa Kila siku Tsh 100
Utapeli mimi nishajua sasa nitakuwa naweka halopesa hiyo vocha sieki.
 
Back
Top Bottom