Halmashauri zilizokopa fedha kutekeleza Mradi wa KKK zatakiwa kurejesha

May 14, 2024
25
20
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI kuhusu Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) unaotekelezwa katika halmashauri mbalimbali nchini kwa fedha zilizotolewa na Wizara hiyo.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati pamoja na Viongozi na wataalam kutoka Wizara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISEMI Mhe. Justine Nyamoga amesema ni vema iangaliwe njia bora kuhakikisha halmaushari zilizokopa na hazijarudisha, zinarejesha fedha walizokopa ili kutoa fursa kwa halmashauri nyingine ziweze kukopa ili wapange, wapime na kumilikisha ardhi katika maeneo yao.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amewahakikishia wajumbe wa kamati hiyo kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Kamati ya Bunge ya TAMISEMI pamoja na Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ili kuhakikisha dhamira ya Serikali ya kupanga, kupima na kumilikisha inatimia kwa nchi nzima.

Pia soma: Waziri Ndejembi aelekeza Watumishi wa Ardhi wasio waadilifu kuchukuliwa hatua

Naye Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amesema mradi huo ni wa nchi nzima, hivyo mikoa ambayo haijaomba kukopeshwa fedha kwa ajili ya kupanga, kupima na kumilikisha maeneo katika halmashauri zao na kuongeza kuwa Wizara imepokea ushauri wa kamati na wataufanyia kazi.

Semina hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

IMG-20240818-WA0036.jpg
 
Back
Top Bottom