KERO Halmashauri ya Hai inatoa vibali ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katikati ya makazi ya watu na kusababisha usumbufu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na ukiukwaji wa sheria za Mipango Mji katika mji mdogo wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai, mkoa wa kilimanjaro.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mazingira wakishirikiana na ofisi ya biashara na ujenzi (ardhi) wamekuwa wakitoa vibali vya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katikati ya makazi ya watu bila kuzingatia sheria za mipango miji.

Baadhi ya maeneo yamekuwa yakipoteza Uhalisia wa mipango miji kwani kumekuwa na kelele za mashine.

Kwa kuwasaidia tu. Watumishi hao warudi kusoma sheria zinazoongoza uanzishwaji wa mji mdogo.
 
Back
Top Bottom