Pre GE2025 Halima Mdee: Nitaenda kumuona Lissu Gerezani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,158
1,984
Mbunge wa viti maalum, Halima Mdee amesema ataenda kumuangalia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu gerezani licha ya mambo yaliyojitokeza baina yake na chama hicho.

Akizungumza akiwa jijini Dodoma jana, Mdee ambaye yeye na wenzake 18 walitimuliwa katika chama hicho amesema ataenda kumuona ili kumtia moyo kwa kile alichoeleza kwamba harakati za upinzani zinahitaji kusaidiana na kutiana moyo.

“Siasa za upinzani zinahitaji kutiana moyo hasa pale ambapo mnapitia mambo magumu kwa mtu alie katika chama tawala hawezi kuelewa hilo, mimi nipo Dodoma lakini nitaenda kumuangalia kama ambavyo Mbowe alipokuwa ndani nilienda kumuangalia”- amesema Halima Mdee.

Chanzo Nipashe
 
Back
Top Bottom