Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Leo Bungeni waziri wa uchumi na uwekezaji, Kitila Mkumbo anawasilisha Hali ya uchumi ya Taifa 2023 na mpango wa maendeleo wa Taifa 2024-2025.
Taarifa hii ndio msingi wa bajeti ya Serikali inayotarajiwa kusomwa baadae leo na waziri Mwigulu Nchemba.
Kaa nami
=======
Waziri Kitila Mkumbo ameanza kwa pongezi ikiwemo spika na wenzake kwa kuendesha bunge la bajeti kwa umahiri. Kitila pia amempongeza Rais Samia kwa kuongoza Taifa kwa weledi, umahiri, uadilifu na utulivu.
Kitila Mkumbo: Mwenendo na muelekeo wa hali ya uchumi nchini

- Mwaka 2023 pato halisi la Taifa lilifikia trilioni 148.3 kutoka trilioni 141.2 mwaka 2022
- Mfumuko wa bei ulifikia 3.1% kufikia Aprili 2024 ikilinganishwa na 4.3% katika kipindi kama hicho mwaka 2023
- Uchumi umekuwa stahimilivu na kukua katika hali endelevu licha ya changamoto zilizoikumba Dunia
- Kuongezeka kwa mauzo nje ya nchi mwaka hadi mwaka, imefikia dola za kimarekani bilioni 8.2 mwaka 2023
- Aina ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi imebadilika katika miongo miwili iliyopita. Mfano miaka ya 2000 asilimia 57 ya mauzo ilihusisha mazao ya kilimo