- Source #1
- View Source #1
Habari zenu wakuu
Hivi nmekua nikijiuliza sana ni hali ya hewa ndio inapelekea watu kuumwa sana sasahivi au ni nini??
Maana nmekua nikishuhudia watu wangi wakikohoa sana ambapo hali hii yakukohoa wengi wamekua wakieleza kua huwakuta sana ifikapo mida ya saa 12 jioni ambayo huwafanya hata washindwe kulala kwa kikohozi icho kikali.
Je, mabadiliko ya hali ya hewa yana mchango wowote katika kusababisha magonjwa?
Hivi nmekua nikijiuliza sana ni hali ya hewa ndio inapelekea watu kuumwa sana sasahivi au ni nini??
Maana nmekua nikishuhudia watu wangi wakikohoa sana ambapo hali hii yakukohoa wengi wamekua wakieleza kua huwakuta sana ifikapo mida ya saa 12 jioni ambayo huwafanya hata washindwe kulala kwa kikohozi icho kikali.
Je, mabadiliko ya hali ya hewa yana mchango wowote katika kusababisha magonjwa?
- Tunachokijua
- Mlipuko wa magonjwa unaweza kusababishwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa, muingiliano kati ya watu wenyewe (au na viumbe hai vingine) pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha, baadhi ya magojwa huwa hayatambuliki asili yake hata baada ya kufanya uchunguzi wa kimaabara.
Pamoja na uwepo wa idadi kubwa ya magonjwa duniani, makundi mawili pekee ya mgawanyiko huu yanaweza kutengenezwa ambayo ni Magonjwa ya kuambukiza na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Kwa mujibu wa WHO, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameshika kasi sana miaka hii ambapo huchangia asilimia 71 ya vifo vyote vinavyotokea kila mwaka duniani. Magojwa ya moyo, saratani, changamoto za mfumo wa upumuaji pamoja na kisukari ndiyo huongoza kwa kushambulia watu wengi zaidi kuliko magonjwa mengine.
Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa ni chanzo kikubwa sana cha kutokea kwa anuai mpya za vimelea vya magonjwa, kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya magonjwa pamoja na kuongezeka kwa vifo, maambukizi mapya pamoja na utegemezi unaotokana na magonjwa haya.
UNEP ambayo ni Idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mazingira inaeleza kuwa uchafuzi wa mazingira unaoenda sambamba na ongezeko kubwa la joto duniani ni kisababishi kikubwa ya milipuko mingi ya magonjwa inayoonekana siku za hivi karibuni.
Mfano halisi wa magonjwa haya ni Dengue, Malaria, homa ya uti wa mgongo pamoja na magonjwa mengi ya mfumo wa fahamu na ngozi ambayo yameongezeka sana kwa sasa tofauti na miaka ya zamani.
Kwenye nyakati hizi ambazo magonjwa mengi yamekuwa yanazuka kila kukicha huku mengine yakiongeza ugumu kwenye kuyatibu, ni vizuri tukianza kutunza mazingira yetu kabla majanga mengine makubwa hayatatokea.
Mtindo wa Maisha yetu ya kila ambayo huwa na athari za moja kwa moja kwenye mazingira inapaswa tuibadilishe sasa.