mwalimu_wa_IT
Member
- Nov 5, 2024
- 42
- 52
Tatizo unafoka saana
Wala sifoki kwa wanao jenga hoja.Tatizo unafoka saana
Maarifa gani?Tafuta maarifa
Hawawezi dunia ina mengi hii wasione watu wanaingia na kutoka tuAu Ile yakufungiwa geto Siku tatu unaoza Siku ya nne ukizinduka ukiona funza ndio pesa hizo , hili zoezi ni la muendelezo pindi pesa zinapopungua
Hii ni Ngumu kumeza atakubali huyu😃
Nitakua lini mkuusema rubi una vituko sana
utakuwa mswahili swahili
Hayo njoo ukamuulize weweHuyo anayekupa hayo masharti ya kunywa damu, Kwanza muulize ana utajiri kiasi gani?
Pia muulize utajiri wake umemfikisha wapi?
Muulize ana utajiri wa kuweza kumzidi walau basi Mo Dewji?
Nimuulize nani?Hayo njoo ukamuulize wewe
Shida stress za home mnaleta jamvini 🙌😂Nimuulize nani?
Huyo anayeulizwa ana hata kampuni yake aliyo isajili kwa jina lake,
Au ndio wale waganga maskini choka mbaya wako kwenye vibanda na matunguli yao wakitafuta wajinga wakuwapiga na kuwadanganya?
Unathibitisha vipi ni mtoto wa 2000?Nilitaka kumjibu hivyo hivyo umeniwahi! Vitoto vya 2000 hivi bwana yani vinajiona vinajua kila kitu kwenye huu ulimwengu, vinadhani kila kitu kinapatikana google
Mimi sina Stress.Shida stress za home mnaleta jamvini 🙌😂
We endelea kupanick achana na wanaodanganywa na waganga
Kazitumie hizo code, walau Uwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk au Jeff Bezos.UTAJIRI (PESA) una code zake (KANUNI) na ndivyo hivyo hivyo kwenye maisha tunayoishi kila siku, nitashusha code za utajiri siku moja.
Siku anakuja shituka alishamaliza ukoo wakeNilitaka kumjibu hivyo hivyo umeniwahi! Vitoto vya 2000 hivi bwana yani vinajiona vinajua kila kitu kwenye huu ulimwengu, vinadhani kila kitu kinapatikana google
Sina mkuu.Mimi sina Stress.
Wewe njoo na hoja na uthibitisho wa uwepo wa huo utajiri wa kishetani acha kupindisha mada.
Basi kama kuna mtu Huwa namuona ni mpumbavu ni yule anayesema hakuna Mungu. Kuna vitu vonatia hasira sana.Waafrika wengi hasa watanzania wamekuwa wakiamini kwa muda mrefu kwamba kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Cha kushangaza hali zao za kiuchumi ziko vilevile miaka nenda rudi.
Kama kweli kwa hakika unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote uwe tajiri mkubwa nchini Tanzania, Afrika na duniani?
Kwa nini ujihangaishe kufanya kazi na kuchoka ilhali unajua kuna utajiri wa kishetani?
Kamtumie huyo shetani akutajirishe kama ni rahisi hivyo!!
Katoe kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako wote tuone kama biashara yako itakuwa kubwa au utaweza hata kufikia utajiri wa Bakhressa.
Kama kweli kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa Afrika kama Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na matajiri wengine wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos?
Kama kweli unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini hujautumia huo uchawi, ushirikina, uganga angalau ufike hata level za utajiri wa Mo Dewji?
Kama unaamini kuna Shetani akitolewa kafara anatoa mali au atakupa mali za kukutajirisha, Katoe kafara wazazi wako au wanao wote tuone kama hata utafika level za utajiri wa Dangote.
Au kama unaamini kuna utajiri wa ndagu, uganga, ulozi n.k
Mwambie huyo mtoa ndagu au mganga, Akupe utajiri angalau umfikie au umzidi Bakhressa kama ana huo uwezo.
Au mwambie huyo mganga akuwezeshe umiliki private jet ✈️, Kiwanda kikubwa cha uzalishaji, Magari makali ya kifahari kama Rolls-Royce Boat tail, Mercedes Maybach, Buggati, Lamborghini, Cadillac escalade au akishindwa sana angalau akupe Range rover sport kwa uganga wake tu.
Waafrika wengi hasa watanzania wana amini kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina lakini bado maisha yao ni ya kimaskini, kikapuku, kifukara pangu pakavu tia mchuzi.
Kama unaamini au unajua kuna Shetani anatoa utajiri, Kamtumie kwa nguvu zako zote akutajirishe na uwe tajiri kweli, Angalau ufike level za utajiri wa kina Dangote.
Kisha ndio uanze kusema kwamba kuna utajiri wa kishetani.
Habari za utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina, Husikika tu kwa waafrika maskini choka mbaya, wajinga, wavivu, makapuku, makabwela na mafukara ambao wanashinda vijiweni na vilabuni waki danganyana na kupeana matumaini uchwara ya utajiri wa kufikirika.
Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani kinacho toa utajiri. Utajiri na pesa hutoka kwa binadamu. Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani chenye pesa.
Pesa ni za binadamu, Si za Mungu wala Shetani.
Hakuna Mungu, Shetani, Jini, Pepo au nguvu yeyote ile ya kimiujiza inayotoa Utajiri.
Pesa, Mali na utajiri hupatikana kwa nguvu za kibinadamu na wanadamu.
Ni wajanja wachache tu huwalaghai na kuwadanganya watu wengine kwamba kuna shetani anatoa utajiri ili kuwahadaa na kuwapumbaza watu wajinga wasiotaka kuhustle wenyewe wakitegemea mafanikio ya kuletewa.
Ndio maana unakuta wanawekewa masharti makali ya kupata pesa hizo ambao wao hudhani ndio masharti ya kishetani ya huyo shetani, Kumbe ni masharti ya binadamu wajanja tu.
The supernatural power is You, Yourself.
Hakuna Mungu wala Shetani anayetoa utajiri, pesa au mali.
I'm out.