Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 25,989
- 62,456
HAKUNA RAHA KAMA KUWA NA MWANAMKE MZURI, MWENYE ELIMU NA PESA ALAFU AWE ANAKUPENDA.
Anaandika, Robert Heriel
Ooh! Sitaki Mwanamke mwenye Elimu,
Ooh! Sitaki Mwanamke anayejiweza kiuchumi,
Hivi mmelogwa? Au hamjiamini!
Hakuna kazi ngumu kama kuishi na Mwanamke asiye na Elimu yaani mjinga.
Na hakuna kazi ngumu kuishi na Mwanamke Maskini au fukara.
Ukitaka kuyafurahia Maisha ya mahusiano ya ndoa, utamu wa Mke au Mwanamke basi awe Mzuri na Mrembo kwelikweli, awe na Akili au hata kielimu angalau Diploma, alafu awe na Mawe kisha akupende. Hakuna Raha utakayoacha kuiona kwenye Hii Dunia.
Kimsingi Sisi wenye Upendo, Wapenda Haki na Ukweli moja ya tabia zetu ni kuishi na watu wakiwa Huru, Mwanamke Maskini Hana Uhuru na kamwe hauwezi kufurahia mapenzi na MTU asiyehuru. Mwanamke asiye na Elimu hawezi kuwa huru kifikra. Ni Watu wa ndio Mzee.
Sisi wengine tunapenda Wanawake wenye utashi, wenye Akili, watakaotuchallenge.
Kama Mwanamke ni Maskini na umemuoa, ukishathibitisha anakupenda;
i) Mpe mtaji au kazi za uzalishaji ajipatie kipato, uone utamu wake.
ii) Mfundishe kuwa na Akili, na vielimu vya hapa na pale. Uone utamu wa kuwa na familia yenye Mwanamke mwenye Akili.
iii) Mpambe apendeze avutie mpaka Roho yako iwe juujuu kama kitanzi cha kunyongea. Uone Raha ya kuwa na MKE.
Usimuogope Mwanamke, hivi unamuogopaje, Ila haimaanishi usichukue tahadhari, hakikisha kila hatua utakayoipiga juu yake umeshaifanyia Calculation na hesabu yake unayo.
Mwanamke ni nyoka mwenye sumu ikiwa hana Akili ya kutosha, ikiwa ni mjinga, ikiwa Hana kipato, ni hatari kubwa.
Ni rahisi kumlaghai Binti Kutoka familia Maskini kuliko Binti Kutoka familia Tajiri.
Ni rahisi kumdanganya Binti ambaye hajaenda shule, yaani Hana Elimu kuliko Binti mwenye Elimu.
Ni rahisi kumdanganya binti wa Kijijini kuliko Binti WA Mjini.
Mwanaume lazima ujifunze kujiamini, na ili ujiamini lazima uwe na Akili, ujanja, hila, mbinu, uzoefu, ustahimilivu, timing, maamuzi magumu n.k.
Unaogopa kuoa Msomi alafu huna sababu za maana, ATI unakiri wazi kuwa utashindwa kum-manage, upo serious Kweli? Kwamba unakiri hauna uwezo na Akili za kutosha kumuongoza Mwanamke mzuri, Msomi, mwenye Mawe.
Unaogopa challenge ya wanaume wenzako? 😂😂
Unaogopa kuchapiwa? Come on! Kuchapiwa kupogo tuu hakuna Guarantee. Ndio maana lazima uweke sheria kuwa ukichapiwa adhabu yake ni kuachana tuu na wala hakuna Mijadala.
Kusema Mwanamke mwenye kipato anadharau, au hana heshima sio sababu yenye mashimo.
Elewa kuwa Mwanamke yeyote anadharau tena dharau kubwa Kwa mwanaume asiyempenda, mwanaume asiyemkoleza na kumkojoza, Kwa mwanaume asiye mjanja mjanja.
Uwapo na Mwanamke yeyote Yule, sheria ya Kwanza ni kuwa na Akili, nazungumzia Akili za kiume ukimix na Ubabe Kwa mbali kama pilipili kuyaendesha mahusiano yako. Ila Ubabe wenye mantiki sio ulete ubabe WA kishamba.
Pili, pendeza, kuwa mtanashati, vutia Wanawake wengine.
Mwanamke mzuri, mwenye kipato, na Elimu licha ya kuwa atakupenda lakini atataka muda wote akuonee Wivu.
Yaani akuone alikubahatisha kuwa na Mwanaume wa Aina yako.
Wanawake wanapenda wakikaa na mashosti zao wasikie waume zao wakisifiwa. Sasa kama mashosti zake hawakusifii unategemea nini hapo.
Wanawake wanapenda Ligi. Wanapenda vitu vizuri au vyenye utukufu.
Wanawake unapowapa Facts hakikisha unaangalia moods zao. Ikiwa moods zao zinaendeshwa na Hisia/mihemko basi TOA majibu ya uongouongo yenye utamu ili kumridhisha.
Ikiwa moods yake yupo katika Akili timamu, basi Mpe Facts zenye mashiko zinazopatana na Akili.
Mwanamke ukimpa facts zisizopatana na Akili yake, yaani anamajibu yenye mantiki kukushinda atakuona hamnazo na ndio mwanzo wa kukudharau.
Ni Bora ukose Pesa Mwanamke atakuelewa na itachukua muda kukudharau. Lakini kamwe usikose Akili, hata uwe na Pesa vipi Mwanamke kama anakuzidi Hoja lazima akudharau alafu akuone hamna kitu.
Yaani hata hizo hela ulizonazo anaona ulizibahatisha au ni majaliwa.
Elewa kuwa Mwanamke anajivunia mwanaume aliyepata utajiri kwa Akili zake sio Kwa bahati bahati.😂😂😂
Mwanzoni ataku- appreciate Kwa sababu ya kipya kinyemi na hajazoea Pesa zako lakini akishazizoea na kugundua kichwani huna kitu, ndio Yale ya kusema mumewe anapesa lakini haridhiki.
Elewa kuwa Mwanamke hatataka kila Siku umzidi, yaani kwenye hoja hakikisha angalau kwenye mijadala 10 basi miwili au mitatu anashinda, Hii itamfanya ajione naye anaakili,
Kumzidi Mwanamke kila Siku ataihesabu kama Ujuaji, u-much know, na ubishi na Wakati mwingine anaweza kujiona kuwa hayupo na MTU sahihi kwake.
Lakini pia epuka kushindwa na Mwanamke kwenye mijadala. Yaani mijadala 10, Mkeo asije kutoa Suluhu yaani mijadala mitano awe ameshinda au amekuzidi. Hiyo ataihesabu kama ameolewa na Mwanaume mjinga, Jambo ambalo hatalivumilia Kwa muda mrefu, dharau itaanza kujitokeza.
Mwanamke mwenye kipato na mwenye Elimu akikupa Pesa usiwe mwepesi kuikubali wala kuikataa.
Kuikataa atahesabu kama haumpendi, Kwa maana ametoa Kwa Moyo WA upendo kama wewe unavyompa Kwa Moyo WA Upendo.
Ukipokea Kwa wepesi bila kuhakiki ataona unapenda kitonga😀😀 mbona hata haujahakiki.
Mfano amekuletea Zawadi ya Kiatu cha Laki tatu. Onyesha kufurahi, onyesha vile anavyokuthamini, Mpe Hug, mwambie unampenda. Kisha muulize ilikuwaje, atasisitiza usijali.
Lakini wewe onyesha kujali kwani alichofanya sio Jambo la kawaida Kwa Wanawake wengi kugusa Bajeti zao kisa waume zao.
Wanawake wanapenda kuambiwa wanafanya mambo ya ajabu, mambo yasiyo ya kawaida.
Mwanamke unapomwambia yeye sio wakawaida na mambo yake sio yakawaida hujisikia Raha. Lakini pia huona kuwa unamjali.
Kitendo cha kuhakiki na kumuonea huruma Kwa kugusa Bajeti yake kisa wewe ataona unamjali na kumpenda.
Elewa kuwa Wanawake hawapendi kuonewa huruma, Ila hapohapo wanapenda, hivyo.
Wanawake wenye vipato, wazuri na wenye Elimu kubwa wanahitaji UPENDO, sio Utumwa na kutumikishwa..
Mwanamke akikupenda na ukimpenda atafanya chochote, nasisitiza chochote, namaanisha, chochote hata kama ni kibaya ilimradi kwaajili YAKO.
Ingawaje niliwahi kusema Wanawake Hawana mapenzi ya dhati, na hii ni Kutokana na sababu kuwa Wanawake hawanaga Uvumilivu WA muda mrefu hasa pale mambo yanapoenda mrama au anapokutana na challenge za nzito.
Zingatia, Wanawake sio Watu wanaopenda vitu vizito hivyo hawawezi kuhimili. Wao ni Watu wa vitu vidogo vidogo, hivyo watahimili.
Uzuri WA Wanawake wazuri, wenye vipato na wenye Elimu ni kuwa hawapendi kuonewa onewa, kunyanyaswa, kukandamizwa, kunyimwa Haki zao.
Jambo ambalo Kwa Sisi Watibeli tunaona ni sawasawa.
Wanawake hawataki Haki Sawa, Hilo hata Mimi nalijua, ingawaje wapo wanaochanganya Haki Sawa na Haki zao.
Wanawake wazuri wenye vipato na wenye Elimu hawataki Haki Sawa kwani wanajua hawataiweza, Ila wanachohitaji ni Haki zao kama Wanawake ili wawe na furaha na waume zao.
Kwa kijana asiyetaka kuwapa Haki zao wanawake, haishauriwi kuoa Mwanamke mzuri, Msomi, na mwenye kipato cha Uhakika kwani hamtawezana.
Kauli ya mwanaume itapingwa na Mwanamke Kwa Arguments, mwanaume kukataa arguments ni dalili ya kuwa Hana hoja na anataka kukandamiza Haki za Familia.
Sisi kina Taikon, Watibeli, ingawaje tunamfumo Dume lakini tunajua mfumo dume tulionao sio wakukandamiza Haki za wengine, ndio maana hatuoni shida kuweka hoja mezani na Wake zetu zikajadiliwa. Kama MKE Atapinga Kwa Hoja zilizozidi hoja zangu basi tutafuata hoja za MKE. Tunajua tunaakili ambazo Mwanamke hawezi kutuzidi Kwa Hoja.
Ingawaje mara mojamoja sio kosa kumpa Mwanamke nafasi ya kushinda ili kile anachotaka kiwe kitokee naye afurahie kuona wazo lake likifanyika.
Mungu tuu ndio hapingwi, lakini Taikon anaamini pia, kuwa hata Mungu Wakati mwingine anatoa nafasi ya mijadala na ikiwezekana kumpinga ikiwa utaona amepuyanga(licha ya kuwa Mungu hapuyangi).
Hiyo ndio maana ya Upendo.
Taikon ngoja apumzike, wale wenye mtizamo tofauti na Mimi nawakaribisha, Mje na hoja. Hiyo ndio vita ninayoiweza na kuipenda. Lakini pia kama mtatumia matusi, nitawajibu kadiri itakavyowezekana na mtakavyokuja.
Umri wangu hauniruhusu kutanguliza Busara.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam