Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
58,995
69,664
Mkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa mitano iliyopo Nyanda za Juu Kusini sanjali na Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Songwe, Njombe na Rukwa. Mbeya ilianzishwa mwaka 1961.

Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe.

Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya.

1. Kiuchumi
Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.

Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.

 2. Hali ya Hewa na Mandhari
Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.

3. Usafiri
Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam. Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa. Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.

4. Kilimo
Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga, matunda, nafaka Hadi pareto na chai.

5. Madini na Nishati
Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2. Umeme ni wa uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.

6. Elimu
Mbeya ni Kati ya Mikoa ya Wasomi hapa Tanzania. Mkoa wa Mbeya una vyuo Vikuu zaidi ya 5 mfano MUST, Mzumbe, CuCoM, UDSM, Tumaini, nk.

Mkoa una mamia ya vyuo vya kati na shule za kutosha eg St.Francis hivyo ni ideal pia Kwa issues za Elimu.

7. Utalii
Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.

Kuna Milima ya Kawetere, bwawa la Mungu, Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahisi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.

8. Viwanda na Biashara
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji, vinywaji vikali na laini kama soda, bia, wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro, vifaa vya ujenzi, home appliances nk.

Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.

Mbeya ndio Kitovu Cha Uchumi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

9. Makazi na Accomodations
Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.

Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa.

10. Watu
Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.

Aidha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.

11. Michezo na Burudani.

Mbeya Ina Wasanii wakubwa Toka kitambo ila icon ya Mkoa ni kina Sugu,VanBoy na Stamina.

Kwenye Michezo hapo ndio nyumbani hususani football.Mbega Ina Timu 3 Ligi kuu za Prisons,Ihefu,Mbeya City na Timu 3 Ligi daraja la kwanza za KenGold,Mbeya Kwanza na Tukuyu Stars.Na Ina Wachezaji Wakubwa wengi tuu na makocha.

Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.








Pia Soma Tukuyu, Rungwe Mbeya wilaya ya kipekee sijaona Tanzania
 
Ntakuja kupaona siku moja ngoja nikusanye nauli si hapo mbeya mjini tu?
Karibu sana never disappoint
Screenshot_20230325-160230.jpg
20230325_155927.jpg
 
Mkoa wenyewe imejengwa hovyo hovyo hasa Mbeya mjini kuliko mkoa mwingine wowote hapa Tanzania. Miundo Mbinu mibovu kuliko mkoa mwingine wowote.

Mbeya mjini wameharibu jiografia kwa kujenga hovyo hadi kwenye vimilima kama kile cha Ilemi, cha Simike! Skwataz everywhere.
 
Back
Top Bottom