Hakimu mbaroni akituhumiwa kupokea rushwa Sh 100,000

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
14,253
23,933
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, David Abel amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kuomba na kupokea Rushwa ya Sh100,000.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 6, 2023, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikes amesema hakimu huyo alikamatwa Aprili 3, 2023, mahakamani hapo.

Wikes amesema hakimu huyo anatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh100,000 tukio ambalo lilifanyika mahakamani hapo, huku akitambua kuwa ni kosa kisheria kufanya hivyo.

"Ni kweli Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Same, alikamatwa Aprili 3, mahakamani hapo kwa kuomba na kupokea rushwa," amesema Wikes.

Aidha Wikes amesema uchunguzi wa tukio hilo umekamilika na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu shtaka linalomkabili.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewaonya viongozi, watendaji na wadau wa mahakama kujiepusha na vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi.

"Mimi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, napinga vita vitendo vya rushwa, nahitaji wananchi wapewe haki bila rushwa. Niwatake viongozi wote wa Serikali na mahakama, wasipokee Rushwa, wawahudumie wananchi na wahakikishe wanatenda haki," amesema Babu na kuongeza.

"Watambue wakipokea Rushwa vipo vyombo vitawaona na watachukuliwa hatua, hivyo kila mmoja atimize wajibu wake bila kuomba na kupokea Rushwa," amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Sijawahi kusikia Majaji na mahakimu wa mikoa hapa Tanzania wakishikwa kwa kupokea rushwa.

Kila siku TAKUKURU inashika mahakimu wa mahakama Za mwanzo tu.

TAKUKURU shikeni nilio wataja ni wapokeaji wa rushwa tena rushwa kubwa.
TAKUKURU ilianzishwa kwa ajili ya wantonge (vidagaa). Ndiyo maana wanaotajwa na CAG wanakula bata tu.

Umaskini ni laana kama kuendesha bodaboda.
 
Sijawahi kusikia Majaji na mahakimu wa mikoa hapa Tanzania wakishikwa kwa kupokea rushwa.

Kila siku TAKUKURU inashika mahakimu wa mahakama Za mwanzo tu.

TAKUKURU shikeni nilio wataja ni wapokeaji wa rushwa tena rushwa kubwa.
Wajanja sana kukamatwa, siyo kama Hawa wa mwanzo
 
Sijawahi kusikia Majaji na mahakimu wa mikoa hapa Tanzania wakishikwa kwa kupokea rushwa.

Kila siku TAKUKURU inashika mahakimu wa mahakama Za mwanzo tu.

TAKUKURU shikeni nilio wataja ni wapokeaji wa rushwa tena rushwa kubwa.
Papa hawezi kula papa boss 😂😂
 
Sijawahi kusikia Majaji na mahakimu wa mikoa hapa Tanzania wakishikwa kwa kupokea rushwa.

Kila siku TAKUKURU inashika mahakimu wa mahakama Za mwanzo tu.

TAKUKURU shikeni nilio wataja ni wapokeaji wa rushwa tena rushwa kubwa.
Kuna Jaji mmoja alikuwa anaitwa jina la kama baba waTaifa, alipokea rushwa Hata Za mauwaji ila hakukamatwa Hata siku moja
 
Screenshot_20230407-154431.jpg
 
Wapuuzi hawa takukuru watu wamepiga mabilioni wanakomaa na ka elfu hamsini wanakera Sana ovyo kabisa
 
Wamemchoka tu, walimtafutia sababu.

Wanashughulika dagaa wanaacha mapapa
 
Sheria ndio huwa zinatumika kwa hawa wachovu wasio na connection, wakati wale wazito wanapiga billions wanachekewa tu.
 
African net,tends to trap small fishes,leaving the bigger ones,passing free.
 
Back
Top Bottom