Chakorii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 18,735
- 51,294
Heri ya mwaka mpya wanaJf.Ninaimani mmeupoea mwaka salama ninyi na wapendwa wenu salama.Kwa upande wangu ninamshukuru Mungu kwani amenichagua tena na si kwa kupenda kwangu bali ni katika mapenzi yake amenichagua.
Wacha niende mojakwamoja kwa kile kilichonifanya nilete uzi.Mwaka 2023 mwishoni hivi nilikaa seat moja na mmama na mtoto wake mdogo katikati ya safari yule mama akaanza kujisikia hovyo basi akaniomba niwe na mtoto wake karibu kwa safari nzima,nilifanya hivyo haïku nikiwa na wasiwasi mwingi nasfini mwangu.Safari ikaendelea huku niisali kwa uzima wa yule mama ili akae sawa Mungo alikuwa mwema sana kariuduma nzuribia ya kufika mama yule akawa ameshakaa sawa basi nikamkabidhi mwanae wakaendelea na safari na akanishukuru sana akizidi kuniombea.tuliachana kila mtu akashika njia yake.
Mwaka jana katikati nikaenda hospitali fulani hivi kupata huduma mara heeee Doctor niliyepangiwa kumuona ndie yule mama niliyemsaidia na kwa bahati nzuri kumbe hata yeye alikkuwa ananikumbuka.Tulizungumza Mengi sana nikapata na huduma nzuri sana na sasa tuko na mawasiliano ya karibu 👏.
Kisa cha pili nilikuwa ninakula maeno ya arusha akaja mlemavu mmoja anaomba msaada wa hela akanunue chakula,ikabidi nimuulize uko na familia?akasema hapana anaishi peke yake nikajisemea sawa.
Badala ya kupatia pesa nikamuomba tukae meza moja tule😊akafanya hivyo tukala pamoja(watu walinishangaa ninauhakika maana yuke mbaba alikuwa mchafu aloo)akafurahi sana na kunishukuru.ikabidi niongee na kiongozi wa hiyo sehemu niliyokula nimlipie yule mbaba chakula kwa wiki.hapo ndipo uwezo wangu ulipokuwa umefikia jaman😁
Sasa pembeni yangu alikuwa amekaa mbaba akiangalia kila kitu mwisho wa siku akazungumza ya kuyazungumza basi mimi huyo nikaondoka zangu✌️siku moja nikaenda ofisi fulani kuna vitu nilikuwa nafuatilia 😳si ninakutana na yule mbaba aliyekuwa akituangalia wakati nakula na yule mlemavu akaniuliza Chakorii una shida gani?nikamweleza kilichonipeleka pale basi akaniambia kaa pale nakuja sasa hivi😊ilichukua kama nusu saa hivi ama dakika 45 akaja yule mbaba akiwa amenikamilishia kila kitu aise🥹🥹sikuamini.akaniambia kitu kimoja ninamnukuu “sister ukiwa kwenye nafasi ya kumsaidia mtu please do”
Nikasema asante nikaondoka zangu.
Kisa cha tatu tena.ilikuwa ni usiku wa kama saa tano hivi nimetoka safari kabla sijashuka katika kituo changu nikampigia boda ambae huwa ninamtumiaga mara nyingi nikamuomba asifunge anisubiri nitachelewa kufika niko safarini.bus lilivyofika nikamkuta boda nae ananisubiri..pembeni yetu kama hatua kadhaa alikuwa amesimama mbaba mtu mzima kiasi akaniomba kwenye hiyo boda tupande nae 😳niliogopa aisee nikamwambia hapana siwezi kupanda boda watu watatu..akasema kama hutojali naomba unisaidie elfu mbili nitafute usafiri maana hapa nilipo sina nauli ikabidi nimuulize boda wangu unamfahamu huyu mtu?akasema ndio ninamfahamu anakaa sehemu fulani nikaona mambo yasiwe mengi nikamwambia hiyo hela ya kukupa sina ila nitaweza kumsort boda, mind you ulikuwa ni usiku na hakuna boda ikabidi nimuombe boda wangu tusubiri kuna rafiki yake alikuwa amempeleka mtu kazini so atapita njia hiyo kurudi nyumbani.tulikaa kama 15 min hivi huyo boda akafika mimi nikapanda boda yangu na yule mbaba mtu mzima akapanda yake akaondoka mbaba alinishukuru huyo kila mtu akashika njia yake huku huyo mbaba akinishukuru.
Ni muda sana umepita juzi hapa rafiki yangu akawa anatafuta frem ya kufungua biashara akapewa number na rafiki yake za mtu mwenye anamalizia kujenga frem zake ziko kama 15 hivi lakini zote zimeshachukuliwa hata kabla hazijamaliziwa.Baada ya rafiki yangu kumpigia mwenye frem simu,mwenye frem akasema hakuna frem yoyote iliyowazi nikamwambia rafiki yangu amuulize huyo mwenye frem kama wanaweza kuonana maana tulisikia kuwa kuna frem nyingine anaanza kujenga ili kama ni kweli rafiki yangu amlipe huyo mwenye frem pesa ili zisije zikaisha.
Mwenye frem akakubaliana aonane na rafiki yangu siku fulani mahali fulani lakini rafiki yangu akaniomba nimsindikize,basi nikamsindikiza wamefika wakaanza kuzungumza biashara zao lakini kabla hawajamaliza yule mzee mwenye frem akaniuliza :
Mzee:binti yangu habari za siku?nikamjibu:nzuri mzee wangu shikamoo.akasema marahaba.
Mzee:Unanikumbuka binti yangu?nikamjibu:hapana mzee wangu kwani tulishawahi kuonana?
Mzee ikabidi sasa aanze kunikumbusha kwanzia mwanzo mpaka mwisho😔mwili wote ukanisisimka aise yule mzee wa kisukuma anajua kutunza kumbukumbu😊.
Surprisingly Yule mzee akamwambia yule rafiki yangu “kwakuwa uko na huyu binti yangu basi Kati ya zile frem 15 mojawapo ilikuwa ni ya kwangu(ya mzee)ya biashara basi ninakupa ufanye biashara miezi mitatu bure utaanza kunilipa baada ya miezi mitatu kuisha”mwisho wa kunukuu.
Na hiki kisa cha tatu kimetokea jana wanaJf wenzangu hakika wema hufungua milango.
WanaJf wenzangu ukipata nafasi ya msaidia mtu mwenye uhitaji basi msaidie ingawa tuko kwenye dunia yenye uwoga na wasiwasi mwingi juu ya binadamu wenzetu na hii ni kutokana na maovu mengi yanayoendelea kutokea.
Heri ya mwaka mpya ndugu zangu
Chakorii ✌️