KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 67
- 129
Kuna jambo ambalo naomba nifikishe hapa ujumbe ili ujumbe huu ufike kwenye Mamlaka za juu, nimeamua kufanya hivi baada ya kuona kile ambacho kimeripotiwa na yule Mwanachama mwingine wa JF kuhusu Shule ya Msingi ya Green Acres ambapo Mwalimu Mkuu anadaiwa kumlawiti Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11.
Kuna Mwalimu wa Shule ya Kingdom Heritage Model School (KHMS) iliyopo Banana Jijini Dar es Salaam ambaye jina lake la kwanza ni Lawrence anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa Miaka 11 ambaye ni Mwanafunzi wa shule hiyo.
Suala hilo limefika Polisi na mtuhumiwa ameshikiliwa lakini taarifa nilizozisikia wanataka kumuachia huku hatma ya mtoto ikiwa haijulikani. Inadaiwa kuna baadhi ya Askari Polisi wanashirikiana na upande wanaomtetea Mwalimu kutaka kulimalia suala hilo kimyakimya.
Inadaiwa wanawaambia kuwa suala hilo ni zito hivyo wanatakiwa wanyooshe mkono ili wao walimalize kimyakimya.
Ninachojiuliza nini hatma ya Watoto wetu kama kuna mwendelezo wa matukio ya aina hii kwenye hizi Shule za Msingi?
Ujumbe huu ufike kwa Waziri Dkt Gwajima, Waziri Mkuu na Rais Samia, huu ni mfano tu wa kinachoendelea mitaani na inawezekana kuna matukio mengi ya aina hiyo yanatokea mitaani lakini hayaripotiwi.
MAMA MTOTO AZUNGUMZA
JamiiForums ilipowasiliana na Mama wa Mtoto kuhusu suala hilo, amesema:
Huyo Mwalimu alimchukua Mtoto akamdanganya kuwa anataka kusherekea naye baada ya kuwa amefanya vizuri darasani, akampeleka nyumba ya wageni, akamfanyia alichomfanyia, baadaye mtoto aliporejea nyumbani akatujulisha.
Tukaenda Polisi, wakatuambia twende Hospitali ya Serikali, akafanyiwa vipimo, baadaye huyo Mwalimu akakamatwa na kuwekwa ndani Kituo cha Stakishari.
Nilipofika Polisi, nilifanikiwa kuonana na huyo Mwalimu (mtuhumiwa), hana la kusema zaidi ya kusema anaomba tu msamaha, Shuleni kwa Mtoto wao tumeonana nao kupitia Mkuu wa Shule na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, wao wanasema wapo pamoja na sisi hadi haki itendeke.
MWALIMU MKUU, DENIS MAGARI:
JamiiForums ilipowasiliana na Mkuu wa Shule ya Kingdom, Denis Magari amesema:
Sina hiyo taarifa, kama suala lipo Stakishari uwaulize Polisi, unataka nizungumze nini?
Hiyo ni jinai, kama limeshafika Polisi waulize hao, hilo ni suala binafsi haijafanya shule, hivyo mimi sina majibu ya kukupa.
Kuhusu kuchukuliwa hatua ndani ya Shule hilo ni suala la Management, kama amekamatwa waulizwe wanaohusika na ajira, mimi sio msemaji wa jambo hilo.
Kwanza hatuna huyo Mwalimu, hilo ndilo jibu la Shule.
Afisa Elimu Wilaya ya Ilala, Magreth Macha
Alipoulizwa na JamiiForums kuhusu shauri hilo, amesema: Suala hilo halijafika ofisini kwangu lakini kama limefika Polisi basi lipo sehemu sahihi.
Suala kama hilo lilitakiwa liripotiwe na Mwalimu Mkuu wa Shule, alitakiwa kuwasilisha taarifa kwetu kisha mchakato mwingine ufuatwe.
JamiiForums ilipohoji kama Mwalimu Mkuu hataripoti kwa maslahi ya Taasisi yake, Magreth amesema: Ngazi ya shule kuna mamlaka ambazo zinahusika kupokea changamoto kama hizo kabla ya kwenda hatua ya mbele.
Pia soma:
~ Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?
~ Dar: Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake afikishwa Mahakamani

===============================