Asante CCM
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 528
- 1,905
Kada na Afisa wa Chama cha Mapinduzi wa zamani ndugu Haji Manara amenukuliwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akisema na nina mnukuu;
" Bandari ya Dar es Salaam ilijengwa na Sultan wa kiarabu toka enzi hizo. Tusijifanye tuna uchungu nayo kivile ilhali haituhusu."
Haji.
Alichoandika Haji Manara
" Bandari ya Dar es Salaam ilijengwa na Sultan wa kiarabu toka enzi hizo. Tusijifanye tuna uchungu nayo kivile ilhali haituhusu."
Haji.
Alichoandika Haji Manara
Wakati huu tukiendelea kujenga hoja zetu DP World Waje au Wasije kuwekeza katika Bandari yetu, tunakumbushana tu Bandari ya Dar es salaam haikuwepo na haikutoka Mbinguni.
Ilianzishwa na kujengwa na Sultan wa kiarabu mnamo mwaka 1843 kabla ya Nchi ya Tanganyika kuwepo wala Mtoto wake Tanzania.
Ni miaka takribani 180 iliyopita, Kiufupi kukosa kina Carl Peters kutengeneza matabaka ya mataifa ya kiafrika mwaka 1884 kule Berlin Germany, Bandari hii ingewahusu Wazaramo na Mashomvi wa Dar tu.
Sina maana hiyoooooooo mnayofikiria lakini ni vizuri tukakumbushana ya zamani pia.
Nb:: Kiuhalisia hii Bandari haituhusu kivileeeeee na kujifanya tuna uchungu kama tumeshushiwa toka Kwa Mungu, kuna Watu walitoa Ardhi yao ya fukwe kisha ukawekwa mzigo ikajengwa those days.
Povu la Team Bandarini ntaoshea Maganda ya Muwa