Haji Manara Amesusa? Hakufurahishwa na matokeo ya Yanga?

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
17,701
37,714
Salamu ni upotezaji wa muda twende moja kwa moja kwenye mada.

Tangu Yanga waibamize Simba 'Kigoli' kimoja huyu msemaji ambaye siku za hivi karibuni alionesha kuitaka sana hiyo kazi.

Hata kupelekea dogo msemaji kujiuzulu.

Leo yupo kimyaaaaaaa hakuna mahali alipojitokeza kuonesha kafurahishwa na matokeo chanya ya club yake ya Yanga. Je amesusa?

Je ametingwa na majukumu mengine? Club imeamua kumweka pembeni na kuacha Ali Kamwe atambe?

Je hakufurahishwa na matokeo ya Yanga?

1723576343985.png
 
Unauliza jambo ulilofikiria ww..
Unadhani yupo wa kufikiri badala yako.
Yani upo umerest sisi ndio tukupe majibu!!
Wewe kama huna majawabu basi wapo wenye nayo kwa sababu jamiiforums ulipo ipo
 
Si alisema Simba atafungwa si chini ya goli 3 sijui. Madogo ambao hata bado hawana muunganiko wakawapelekea mafaza moto hatari wakaambulia kimoja tena na chenyewe wamepewa na Kapombe.

Kina Pacome aliyempamba sehemu zake juu ya magoti atakuwa amemwambia ebwana eeeh, tumeshinda ila cha moto tumekiona.
 
Mbona una harufu ya Ahmed semaji?
 
Si alisema Simba atafungwa si chini ya goli 3 sijui. Madogo ambao hata bado hawana muunganiko wakawapelekea mafaza moto hatari wakaambulia kimoja tena na chenyewe wamepewa na Kapombe.

Kina Pacome aliyempamba sehemu zake juu ya magoti atakuwa amemwambia ebwana eeeh, tumeshinda ila cha moto tumekiona.
Mbumbumbu katika ubora wake. Hivi sijui unaonekanaje na una umri gani? Inawezekana hapo mtaani unspoishi kuna watu wanakuheshimu na kukuona wa maana sana kumbe humu JF ni Mbumbumbu na Juma Kilaza tu.
 
Manara hana raha! Manara alitarajia kupokelewa kwa shangwe na vifijo huku akisindikizwa na mashada ya maua! Kwa bahati mbaya, hasa kule Instagram ambako Manara yupo active, asilimia kubwa ya comments za mashabiki wa utopolo walionesha kumhitaji zaidi Ally Kamwe kuliko Manara!
 
Huwenda ikawa sababu?
 
Alisikika wasafi FM akiahidi simba akipona chini ya Goli 4 atatoa Millioni moja moja kwa kila Presenter wa kile kipindi
 
Mwacheni mwana simba mwenzetu yule yuko yanga kimasilahi tu ila moyo uko Simba🤣Sawa na dem anayekupenda ila pia anapenda pesa.
 
Viongozi watakuwa wamefanya la maana sana, timu iende ki professional. Wewe mtu mpo kwenye vitu serious tena watu wenye wadhifa na heshima zao wanafuatilia yeye anakomaa na Mobeto aje atambulishwe na Azizi Ki pia mdomo wake umemfanya awe mtu wa kutengeneza maadui na sio ujamaa, kule goal.com walipost hadi ishu ya Manara kuwa kejeli Kaizer Chiefs kisa kufungwa goli nne na Yanga na mashabiki wakamaindi. Huyu anatakiwa akae mbali na Yanga
 
Back
Top Bottom