Haji Manara amepunguziwa adhabu ya Faini kutoka milioni 20 hadi milioni 10

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,941
2,043
Kamati imetangaza mapema leo kwamba Haji Manara atapunguziwa adhabu yake aliyopewa awali. Kwenye suala la hela imeshuka kutoka ilipokuwa awali milioni 20 hadi milioni 10 na azilipe ndani ya siku 30, ila miaka miwili ipo palepale.

Full story:
---
1663326816703.png

Picha: Haji Sunday Ramadhan Manara

Msemaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amepunguziwa adhabu ya Faini kutoka Milioni 20 hadi Milioni 10, huku hukumu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili ikibaki palepale.

Maamuzi ya kumpounguzia adhabu Manara yametangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF Richard Mbaruku jana Jumatano (Septemba 14) majira ya Usiku.

Richard Mbaruku amesema Kamati yake imepitia Rufaa ya Haji manara na imeona haina mashiko lakini, lakini imelazimika kutumia busara kumpunguzia adhabu ya Faini.

Kamati ya Rufaa imemtaka Haji Manara kuhakikisha analipa faini hiyo ndani ya siku 30, baada ya kutangazwa kwa maamuzi ya Rufaa aliyoiwasilisha mbele yao.

July 21 Mwaka huu 2022, Haji Manara alitangazwa kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na Faini ya milioni 20 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF Wallace Karia wakati wa mchezo wa Fainali Kombe Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Young Africans dhidi ya Coastal Union, uliopigwa jijini Arusha July 02.

Tuheshimu mamlaka na pia bado ana nafasi ya kwenda ngazi za juu kukata rufaa..
 
Tff ni wahuni tuu ndio maana Taifa Stars haieleweki wao wamejikita kwenye mambo ya hovyo hovyo na kuacha mambo ya msingi kabisa kwao mambo ya kijinga ndio hoja kuu.

Hatuwaoni kuwa na kamati za Maendeleo ya soka la Tanzania kwa vijana na wengine kuwafanyia mpango kucheza Academy kwenye Timu za Ulaya hata Timu ndogo ukiona mtu yupo nje ni kwa nguvu zake wao ni manara mara usajili sijui wa BM 23 miaka nenda rudi wakiamka utasikia kufungia waandishi wa habari..kwa akili hizo kusimamia soka tutafungwa sana na majirani zetu.
 
Tff ni wahuni tuu ndio maana Taifa Stars haieleweki wao wanejikita kwenye mambo ya hovyo hovyo na kuacha mambo ya msingi kwao mambo ya kijinga ndio hoja kuu...hatuwaoni kuwa na kamati za maendeleo ya soka la Tanzania kwa vijana na wengine kuwafanyia mpango kucheza Academy za nje wao ni manara mara usajili sijui wa BM 23 miaka nenda rudi wakiamka utasikia kufungia waandishi wa habari..kwa akili hizo kusimamia soka tutafungwa sana na majirani zetu...
Inasikitisha. Tena walivokosa aibu tamko wamelitoa saa ngapi unajua? Saa 7 au 8 usiku ilikuwa ile
 
Haji Manara, mimi siyo shabiki wako! Ila linapokuja suala la kupambania haki, hakika nitaungana na wewe. Usitoe hata 100 kwa hao wapigaji! Wewe na Karia mlilumbana kwenye mambo yenu ya kipuuzi.

Hivyo huo upuuzi wenu ulitakiwa uishie palepale uwanjani, siku ile ya fainali. Hakukuwa na sababu ya kushtakiana, na wakati hata huyo Karia mwenyewe siyo mtu wa staha! Maana anafahamika na yeye ni mropokaji tu na msema hovyo kama wewe!!

Usawa huu na hela ilivyokuwa ngumu! Kirahisi tu uwape hao wapiga dili milioni 10, ili wakaendelee kujaza vitambi vyao pale TFF! Huku wewe mwenyewe na huo ulemavu wako, ukipambana usiku na mchana kutafuta hizo hela kupitia huo mdomo wako usioweza kuchuja maneno ya kuongea!

Sikushauri aisee!! Pambana nao mpaka kieleweke.
 
Haji Manara, mimi siyo shabiki wako! Ila linapokuja suala la kupambania haki, hakika nitaungana na wewe. Usitoe hata 100 kwa hao wapigaji! Wewe na Karia mlilumbana kwenye mambo yenu ya kipuuzi.

Hivyo huo upuuzi wenu ulitakiwa uishie palepale uwanjani, siku ile ya fainali. Hakukuwa na sababu ya kushtakiana, na wakati hata hiyo Karia mwenyewe siyo mtu wa staha! Maana anafahamika na yeye ni mropokaji tu na msema hovyo kama wewe!!

Usawa huu na hela ilivyokuwa ngumu! Kirahisi tu uwape hao wachumia tumbo milioni 10, ili wakaendelee kujaza vitambi vyao pale TFF! Huku wewe mwenyewe na huo ulemavu wako, ukipambana usiku na mchana kutafuta hizo hela kupitia huo mdomo wako usioweza kuchuja maneno ya kuongea! Sikushauri aisee!! Pambana nao mpaka kieleweke.
😂😂 Bro, mbona kama upo upande wa Karia?
 
Haji Manara, mimi siyo shabiki wako! Ila linapokuja suala la kupambania haki, hakika nitaungana na wewe. Usitoe hata 100 kwa hao wapigaji! Wewe na Karia mlilumbana kwenye mambo yenu ya kipuuzi.

Hivyo huo upuuzi wenu ulitakiwa uishie palepale uwanjani, siku ile ya fainali. Hakukuwa na sababu ya kushtakiana, na wakati hata huyo Karia mwenyewe siyo mtu wa staha! Maana anafahamika na yeye ni mropokaji tu na msema hovyo kama wewe!!

Usawa huu na hela ilivyokuwa ngumu! Kirahisi tu uwape hao wapiga dili milioni 10, ili wakaendelee kujaza vitambi vyao pale TFF! Huku wewe mwenyewe na huo ulemavu wako, ukipambana usiku na mchana kutafuta hizo hela kupitia huo mdomo wako usioweza kuchuja maneno ya kuongea!

Sikushauri aisee!! Pambana nao mpaka kieleweke.
Mshawishi asitoe hiyo hela ili nafasi ya usemaji Yanga uichukue wewe kabisaa
Nimependa mbinu yako mkuu
 
Huyu mbwa wangemfutia kabisa adhabu ya faini badala yake wangemuongezea adhabu afungiwe maisha kujishughulisha na mpira wa miguu
 
Attachments

  • JamiiForums-1514843452.png
    JamiiForums-1514843452.png
    224.9 KB · Views: 6
Back
Top Bottom