Tunataka aliekurupuka wa kutoa amri ya vunjavunja awajibike au awajibishwe kwani serikali inatakiwa kufuata sheria na haswa ilivyokuwa serikali ni mpya na imeingia madarakani hata miezi mitatu haijatimia.
Mtu alietoa amri ya vunjavunja alikuwa na haraka gani ? Au akijitafutia umaarufu ? Je kama ungepita uchunguzi wa kimagufulism ,hio fidia si ingepungua kuliko sasa ,maana kama mtu alikodi guest alilala inje na anaendelea kulala nje na watoto wake wachanga hivi fidia ya kisaikolojia hapo italipwa vipi ?
Baada ya makelele na vilio ndio serikali hii mpya inakumbuka kama kuna vibali au hakuna ,kwanini kabla ya kukurupuka na kujitafutia umaarufu haikujiridhisha kuwa waliojenga hapo hawana vibali .ilikuwaje wakafikishiwa miundo mbinu ya umeme na maji nani alitoa amri hio?
Unyanyasaji ndio huu ,serikali ilikosa hekima na busara na badala yake kupitisha kimbunga ilichokitengeneza, mhusika alietoa amri kama ni raisi au waziri basi ni kuomba samahani kwanza na kuwafariji waathirika wa kimbunga hicho iwe wananchi hao wana vibali au hawana.