Naomba serikali ijaribu kutusaidia kuwaondoa vishoka na matapeli wote waliopo katika office za TRA, wamejaa sana kiasi kwamba ukifika pale kidogo ukiulizia office yoyote pale mapokezi anatokea mtu anajifanya kama anataka kukusaidia, sasa apo atakupa michanganuo ya kukupiga pesa
Hivi ni kweli kabisa TRA mmeshindwa kuweka michanganuo ya kodi fulani inatakiwa ilipweje, naomba mtu saidie maana watu wengi katika huduma zenu tunashindwa kuzipata kutokana na office zenu kuzungukwa na vishoka na matapeli pale nje na mule ndani katika kolido zote. Kuna watu wengi wanashinda kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Kingine cha mwisho ukifanikiwa kufika sehemu husika uwezi kupata huduma utaambiwa mtandao haupo. Lakini wakifika vishoka na matapeli wanaacha zile fomu zao wanafanyiwa kazi, wafanyakazi wote waliopo TRA office wanajua kwamba pale kuna vishoka na matapeli. Na ndio maana watu wengi wanshindwa kupata huduma.
Leo nimeenda pale TRA office nimekaa siku nzima akuna cha huduma wanadai mtandao haupo, hivi kweli kwa mwendo huu watu wengi wataweza kulipa kodi kweli
Nawasilisha....