Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,836
- 1,580
===
Mtakumbuka Rais wa Kenya William Ruto, aliagiza kusitishwa kwa kandarasi ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa JKIA na ya nishati iliyopewa kampuni ya Adani kutoka India.
" Naelekeza kwamba...wakala wa ununuzi ndani ya Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Uchukuzi. Nishati na Petroli zisitishe mara moja, mchakato unaoendelea wa shughuli ya upanuzi wa uwanja wa JKIA ambao ni ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi,pamoja na mkataba wa usambazaji wa njia za umeme wa kampuni ya KETRACO uliohitimishwa hivi karibuni na mara moja kuanza mchakato wa kuhusisha washiriki wengine," aliagiza Rais huyo.
Mwezi Julai 2024 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Kenya (KAA) ilithibitisha nia ya kampuni ya Adani kuhusishwa kwenye upanuzi wa uwanja wa ndege wa JKIA, licha ya kampuni hiyo kutopewa kandarasi yoyote .
Haya yote yanajiri huku mamlaka moja nchini Marekani ikimshtaki mmiliki wa Kampuni ya Adani Holdings Limited ya India, bilionea Gautam Adani na watendaji wengine saba kwa tuhuma za rushwa na ulaghai wa dhamana kwa majukumu yao katika mpango wa mabilioni ya dola ili kupata fedha kutoka kwa wawekezaji wa Marekani na taasisi za kifedha duniani.
Washitakiwa hao ni pamoja na Adani, Sagar Adani na Vneet Jaain, watendaji wa kampuni ya India ya nishati mbadala ya Indian Energy Company.
Mkataba kati ya kampuni ya Adani na Kenya wa usambazaji ya umeme unagharimu zaidi ya dola milioni 700 ambao pia ulikuwa umeidhinishwa na Wizara ya Nishati ya Kenya.
Oktoba mwaka huu,
Kampuni ya Adani Energy Solutions ilitia saini mkataba wa miaka 30, wa dola milioni 736 wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi na Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Kenya.
Mahakama nchini Kenya ilihairisha mkataba huo mwezi huo wa Oktoba.
Hata hivyo Kampuni ya Adan Group imejitokeza hadharani ili kukanusha kuwa na Mkataba wowote wa kuendesha uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta badala yake wamekubali kuwa na Mkataba wa Kusambaza Umeme na Ujenzi wa station 2 za Umeme ambao hata hivyo.Adan Group imesema mkataba huo hauangukii kwenye Sheria zozote za Kimataifa na India zinazoweza kutoa mwanya kwa mamlaka za Kenya kuuvunja kutokana na tuhuma na makosa yaliyofanywa India na kufunguliwa kesi Marekani kwa hila.
Pia soma https://www.business-standard.com/a...group-124112300996_1.html?print=1&isFree=true
Hata hivyo Rais Ruto hakuweka na hajaweka bayana endapo mkataba mwingine unaoendelea kutekelezwa wa zaidi ya Sh 104bn wa huduma za afya nchini humo baina ya Adani Group na nchi yake ya Kenya kama nao utavunjwa au laa?
1. Je, TANZANIA tunamkataba wowote wa PPP wa kuuvunja au laa?
2. Je, Kenya inamkataba wowote na Marekani wa maswala ya kiulinzi na kibiashara iliousaini kwa Siri na haya ndio matokeo yake?
3. Je, TANZANIA ifuate njia ya Kenya au isimame tu katika Sheria na taratibu ilizojiwekea kwenye PPP?
Chakustaajabisha ni kuwa kampuni za Adani Group tangu sekeseke hilo limpate na lipambe moto kampuni hizo zimepata hasara ya zaidi ya US$34bn karibu TZS 88.5Trilioni, unaambiwa hii ndio maana halisi ya vita za kibiashara za kampuni kubwa kubwa duniani.
View: https://youtu.be/KA69rQP8vic?si=Z7WKLgMR-Q18eNsA