Guiness World Records wagoma kutambua rekodi ya Land Rover Festival ya Tanzania

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,823
5,435
Kwa jinsi wachuganistan walivyojiandaa na Land Rover Festival, na jinsi Media zilivyosapoti tukio hili zito, ni jambo la kushangaza kwamba Guiness World Records wameshindwa kutambua rekodi hii iliyovunjwa na watu wa Arusha, ya msafara wa magari zaidi ya 1000. Mpaka hivi sasa hawajazungumza chochote juu ya Rekodi hii ya Dunia.

Ikumbukwe kuwa rekodi ya msafara mkubwa zaidi wa magari ya Land Rover iliyotambuliwa rasmi na Guinness World Records ilifanyika Julai 2018 katika Maonyesho ya Billing Off-Road mjini Northampton, Uingereza. Hafla hii ilikusanya jumla ya magari 908 ya Land Rover, ingawa ni magari 640 pekee yaliyoafikia vigezo na masharti makali yaliyowekwa na Guinness. Sheria hizo zilihitaji magari kuachiana nafasi maalum na kuwa na mwendo thabiti katika msafara, jambo lililoleta jumla iliyothibitishwa ya kuvunja rekodi na kuwazidi wale walioweka rekodi ya awali ya magari 632 nchini Ujerumani mwaka 2017.

Msafara huo ulijumuisha matoleo mbalimbali ya Land Rover kuanzia ile ya zamani ya mwaka 1955, Series I, hadi modeli za kisasa zenye teknolojia ya kisasa ya hybrid, ikionyesha historia ndefu ya brand hiyo. Kampuni ya Lancaster Insurance ilisaidia hafla hiyo, ikishiriki msafara na gari jipya la Discovery kwa kuadhimisha miaka 70 ya Land Rover na msafara wa kusisimua wa wapenzi wa brand hiyo.

Je hili Convoy la Land rover hapo Arachuga liliwakilishwa na nani kutoka Guiness World Records, au watu walivunja record kwa kujiamulia. Je ni vigezo vipi viliwekwa hili kukizi sheria za kuvunja Record. Isije ikawa Gari ni Land Rover lakini Engine ya Subaru, alafu mnataka muiite Record Breaking.



View: https://youtu.be/56Q4SP5qrRw?si=2XNdlcYLgP2eS6SQ
 
Impact ya kula nyama kuchenyetah showuofu nani ana pisi kali nani kabeba pombe za bei ya juu nani karundika bia nyingi kushinda wenzake.....teh teh teh

Mge gawa dafutari na pencil moja moja kwa kila shule mnayopita MGEFIKRIWA....mmeacha madeni huko mpaka mnafikishana unjaguni

Ilikuwa nafasi nzuri ya kufanya Fundraising ya kukuza elimu Northern TZ kupitia hizo Ndorofah nexttime mutumie BRAIN leo mgekuwa na mfuko wenye Mabilioni ya kutosha kusaidia watoto huko Mashuleni
 
Hata kama Guiness ikibisha Rekodi ya dunia ndio imeshawekwa na kwa utandawazi wa sasa dunia ishajua zamani sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom