Gridi ya Taifa yapata hitilafu na kusababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme, TANESCO watoa taarifa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,330
4,692
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa Wateja wake kuwa kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa majira ya 08: 40 usiku May 04 20224 na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme kwenye baadhi ya maeneo iliyounganishwa na Gridi hiyo.

TANESCO wanasema Juhudi za kurejesha umeme zinaendelea kwa haraka ili huduma iweze kupatikana katika maeneo yote yaliyoathirika, na baadhi ya mikoa kama Dodoma na Iringa zimeanza kurejea.

Shirika linawaomba uvumilivu Wateja wake wote wakati Watalaamu wakiendelea na jitihada za urejeshaji wa mfumo wa Gridi ya Taifa.

1714786118376.png

Pia soma: Hitilifafu za Gridi ya Taifa ndani ya mwaka 2024
 
Enzi za Mkapa na Magu, Gridi ikizima ni sawa na jaribio la kupindua nchi, wahusika wanaenda kujieleza mjengoni!

2024 pekee tu, gridi imechomoka mara ngapi? Wako serious kweli?
  • Hitilafu maana yake ni nini?
  • Nguzo zikianguka, inasemwa, wandhani hatuna akili ya kujua watachosema? Na itokee sasa hata kama wanajua tatizo ni nini!

Ninachojaribu kusema, upumbavu umezidi kukithiri! Kucheza na hatima ya maisha ya watu ndio dili la panya wachache walioko chamani na serikalini!

Huhitaji vyombo vya habari kujua nchi iko gizani, hatukuwa na hii mambo kipindi fulani....mtasema ilikuwa inatokea ila waliogopa kusema?
 
View attachment 2980285

Pia soma: Hitilifafu za Gridi ya Taifa ndani ya mwaka 2024

U naibu waziri mkuu ungefutwa tu, ni mzigo usiokuwa na tija yoyote kwa Taifa.
 
Enzi za Mkapa na Magu, Gridi ikizima ni sawa na jaribio la kupindua nchi, wahusika wanaenda kujieleza mjengoni!

2024 pekee tu, gridi imechomoka mara ngapi? Wako serious kweli?
  • Hitilafu maana yake ni nini?
  • Nguzo zikianguka, inasemwa, wandhani hatuna akili ya kujua watachosema? Na itokee sasa hata kama wanajua tatizo ni nini!

Ninachojaribu kusema, upumbavu umezidi kukithiri! Kucheza na hatima ya maisha ya watu ndio dili la panya wachache walioko chamani na serikalini!

Huhitaji vyombo vya habari kujua nchi iko gizani, hatukuwa na hii mambo kipindi fulani....mtasema ilikuwa inatokea ila waliogopa kusema?

Walipo watakuwa wanaangalia namna ya kukitumia kimbunga "Hidaya" kama fursa
 
Changamoto kubwa kuliko yote ni kukosa wataalam wa vitendo (maarifa). Tupo vizuri kwenye maneno na maombi (ambayo pia Mungu hasikilizi watu waliokosa maarifa).
Tunazalisha na kuajiri watu wa maneno zaidi.
 
hizi taaarifa za kukatwa tunazo saa mbili usiku angalia updates za hidaya na nkashauri mpigepasi mapema msikose ibadan ya jumuiya...nimewapemda n tym hidaya anaongeza speed nao chap wakakata

Kwa usalama wetu nawapongeza maana sijalala vioo vya madirisha kama vibataka kuondoka 📳
 
Back
Top Bottom