Graphics Designer naomba natafuta kazi

Ivan Breaker

JF-Expert Member
Jun 13, 2020
1,379
5,495
Habari za jioni ndugu zangu! Nimekuja kwenu hapa kuomba Support ya aina yoyote katika kitu nachokifanya cha kujitafuta na kutafuta maisha kusudi mambo mengine yaweze kwenda vizuri.

Nimekuwa nikifanya kazi za Graphics designing pamoja na kazi za uPhotographer lakini changamoto kwangu imekuwa ni upatikanaji wa vitendea kazi kama laptop pamoja na camera.

Vyote hivi nimekuwa nikiazima na muda mwingine nikipata kazi za graphics nimekuwa mtu wa kuzunguka sana kwa rafiki zangu wenye Laptops na computer kitu ambacho kinanikatisha tamaa hata ya kuendelea kufanya shughuli hizi lakini bahati nzuri au mbaya, nimekuwa na mapenzi makubwa sana na kazi yoyote inayohusisha utumiaji wa camera au laptop/ computer.

Pia nimekuwa nikifanya vyote hivi bila kupita kwenye shule yoyote ile wala bila kupata short course yoyote zaidi nimekuwa nikijifunza mwenyewe kupitia mitandao tu na namshukuru Mungu kwa sasa naweza kufanya kazi zaidi hata ya mtu yule aliyeenda kusoma hizi short course za mtaani.

Support nayohitaji ni kupata sehemu ya kufanyia kazi hata kwenye ofisi ya mtu yeyote aweze kuniajiri kama kijana wake nifanye kazi kwake. Pia niweze kupata support yoyote ile kwa mtu atakayeguswa na hili jambo.

Uzoefu wangu upo kwenye utumiaji wa camera, kufanya editings pamoja na kufanya manipulation kwa uchache, naweza pia kufanya graphics yoyote inayohusisha kutumia Adobe Photoshop na siku za karibuni nimekuwa nikijifunza na kufanya kazi za motion graphics kwa kutumia After Effect.

Nina uzi ambao umebeba kazi zangu na pia kuna kazi ambazo zipo kwenye mfumo wa video, hizo zenyewe zinapatikana kwenye Instagram yangu @realivanbreaker

Asanteni!

Baadhi ya kazi zinapatikana kwenye uzi huu hapa chini

Karibu tushirikiane View attachment 2451835
InShot_20221215_131848608.jpg
 
Nashukuru pia ningependa unikosoe palipo na makosa ili nijuwe wapi pakufanyia marekebisho

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
Kuanzia apo ulipoandika jipatie umeshindwa kuchagua rangi inayoendana ikaleta mvutor,pia bango lako Dogo lkn umelijaza maneno mengi,jitahid kuchagua fonts nzuri kulinganisha na ukubwa wa bango lako,picha za msosi nyingi (3 ) kulinganisha na bango husika au ulipaswa ziwe ndogo kiasi kama ulitaka kuweka zote 3 badala ya 2, jitahid kuchagua rangi na fonts ambayo itakuwa visible kwa mtu kusoma bila kupata shida na kumvutia msomaji ,hakikisha bango lako unapoliandaa maneno yako hayafichi picha au yakawa interacted na picha uliyolenga ionekane ili ivutie watu uliowalenga

Sent from my CPH2325 using JamiiForums mobile app
 
Sawa sawa nitalifanyia kazi hili

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom