Jamiitrailer
Member
- Oct 20, 2019
- 56
- 161
Wadau, hii mada ishajadiliwa sana baada ya serikali kutoa tamko kwamba Malawi inafunza watoto kupitia ramani za google ambazo zinaonesha ambazo zinaonesha ziwa lote ni milki ya Malawi.
Ukweli ni kwamba ramani zote za Google (map & earth) hazioneshi hivyo.
Mpaka wa ziwa Nyasa kati ya Malawi na Msumbiji umepita katikati ya ziwa, kiasi kwamba ili Malawi wafike katika visiwa vyao viwili vya Likoma na Chizumulo inabidi kwanza waingie maji ya ziwa yanayomilikiwa na Msumbiji.
Mpaka unaotenganisha Msumbiji na Malawi unaoneshwa kiramani kama straight line kijiografia kuashiria mpaka wa kimataifa unaoeleweka.
Hicho kinachodaiwa kuwa ni mpaka unaotenganisha Malawi na Tanzania,umepita upande wa kulia na kuligusa eneo lote la ziwa eneo la upande wa Tanzania, lakini alama ya kijiografia iliyotimiwa na Google ni ile ya dot..dot katika kuonesha kwamba mpaka husika siyo definitive, yaani Mpaka haujajulikana rasmi.
Kwa hiyo ramani Google hawajaonesha kinachodaiwa.
Isitoshe,Malawi wanafundisha watoto wao ramani za kuonesha ziwa lote ni lao hata kama siyo hali halisi toka miaka ya nyuma kabla ya Google kuweko.
Soma Pia: Serikali: Marufuku Kutumia Ramani ya Tanzania kutoka Google Kufundishia Wanafunzi, Inaonesha Ziwa Nyasa liko Malawi
Kimsingi,kwa sheria za kimataifa Tanzania ina haki ya kuwa na sehemu hiyo ya ziwa ambayo wananchi wake wameishi pembezoni, ambapo kwa shughuli zao za kiuchumi na mtindo wa maisha na tamaduni kiujumla vimejijenga kutokana na ziwa kwa vizazi na vizazi kabla ya wakoloni kuingia Afrika.
Wananchi hao wasipokuwa na haki ya kutumia maji hayo na kulazimika kubadilisha mfumo wao wa maisha kwa kuambiwa kwamba kuna mmiliki wa maji yuko upande wa pili wa ziwa kuzuia matumizi, wakati sheria za kimataifa zinataka mpaka wa maji uwe katikati, itakuwa ni vichekesho.